Halmashauri zote Nchini zimetakiwa kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya Mapato
Na; Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
—————————
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
amezitaka Halmashauri zote Nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika
kukusanya mapato kuanzia Julai 01, 2016.
Mhe. Majaliwa aliyasema hayo
Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la
kumi na moja Juni 30, 2016.
“Napenda kutumia fursa hii
kuziagiza Halmashauri zote Nchini kwamba kuanzia tarehe Mosi Julai, 2016
zihakikishe zinatumia mifumo ya kieletroniki katika kukusanya mapato,
katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya
kuboreshha makusanyo,” alifafanua Mhe. Majaliwa
Aidha Mhe. Majaliwa amezitaka
Halmashauri hizo kutoelekeza vyanzo vyote vya mapato kukusanywa na
mawakala kwani vipo vyanzo ambavyo vinaweza kukusanywa kwa ufanisi na
Halmashauri zenyewe bila kutegemea mawakala.
Aliendelea kusema kuwa,
Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia
mawakala na vingine vitakusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia
miongozo iliyotolewa na Serikali.
Mhe. Majaliwa aliitaja miongozo
hiyo kuwa ni pamoja na Halmashahuri aidha kwa kutumia mawakala au
Halmashauri zenyewe kuweka kwenye akaunti ya Halmashauri fedha zote
zinazokunywa kwa kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza na
kumaliza kabisa masuala ya (cash transactions).
Vile vile Halmashauri zikubaliane
na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala
na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya
Halmashauri.
Sheria ya Fedha ya Serikali za
Mitaa sura 290, inazipa uwezo mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa
kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya
mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Sheria hiyo pia inazipa mamlaka
hizo kuteua Mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni