Kupinga utumikishwaji wa watoto si jukumu la serikali pekee
………………………………………………………………………………………..
Benjamin Sawe-Maelezo.
Utumikishwaji
wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo kutokana na tawkimu za
makadirio za mwaka 2000-2012 za Shirika la Kazi Duniani asilimia 11
(watoto milioni 264) ya watoto wote duniani wenye umri wa miaka 5-17
wnatumikisahwa kwenye ajira za aina mbalimbali sawa na asilimia 11 ya
watoto wenye umri huo.
Kwa
upande wa Tanzania, utumikishwaji wa watoto kwa mwaka 2014/15 matokeo ya
utafiti yanaonesha kuwa kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya
miaka 5 hadi 17 (watoto milioni 4.2) sawa na asilimia 28.8
wanatumikishwa katika kazi mbalimbali
Takwimu
hizo zinaonesha kuwa sekta za kilimo na uvuvi zimeendelea kuwa sekta
zinazoajiri watoto wengi zaidi ikiwa ni kiwango cha asilimia 92.1 ya
watoto wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi na wengi wao wanaishi
vijijini.
Akizungumza
katika uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa
watoto Tanzania Bara wa mwaka 2014, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt. Albina Chuwa anasema matokeo ya utafiti huo yanaonesha
kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao wa siku ikiwa ni asilimia
58.8 kwa shughuli za kujihudumia na usafi huku wasichana wakionekana
kutumia muda mrefu zaidi kwa shughuli hizo kwa kiwango cha asilimia
58.3.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni