CHUKI ZIKO KATIKA SIASA SIO MPAKA URAIANI !!
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa 
CCM Taifa Mh. Nape Nnauye na Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa 
Chama cha CHADEMA wakijadiliana jambo wakati alipokutana katika shughuli
 ya kuaga mwanahabari Mpiga Picha Marehemu Joseph Senga aliyefaiki 
mwishoni mwa wiki hii Nchini India alikokuwa akitibiwa maradhi ya moyo  
shughuli hizo za kuaga mwili wa Marehemu Joseph Senga zimefanyika Sinza 
na mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Kwimba mkoani Mwanza 
kwa mazishi.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa 
CCM Taifa Mh. Nape Nnauye akizungumza na Mh. Edward Lowasa Waziri Mkuu 
wa Zamzni na kada wa CHADEMA katikati kushoto ni Kada mwingine wa 
CHADEMA Ndugu Khamis Mngeja.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni