MHADHIRI WA CHUO KIKUU-UDSM ANYAKUA TUZO NNE ZA FILAMU ZIFF 2016
………………………………………………………………………………………….
Usiku wa jana ulikuwa 
ni wa furaha ya aina yake kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakiwania tuzo 
kwenye tamasha la kimataifa la filamu la ZIFF lililofanyika Zanzibar na 
miongoni mwa washindi hao ni Amil Shivji,ambaye pia ni mwalimu wa 
masuala ya uandaaji filamu kwenye idara ya sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar 
Es Salaam.
Bw.Amil kupitia filamu 
ya AISHA iliyotengenezwa na kampuni ya Kijiweni Production kwa 
ushirikiano na shirika la Uzima kwa Sanaa(UZIKWASA) lilipo Tanga,kwa 
ujumla ilijishindia tuzo takriban nne katika kipengele 
kilichoshindanisha filamu za kiswahili, maarufu kama “bongo movie”.
Filamu ya AISHA 
iliyotengenezwa Pangani-Tanga, imekwishachezwa kwenye zaidi ya matamasha
 thelathini(30) duniani, iliweza kuibuka kinara kwenye ZIFF kwa kutoa 
muongozaji bora(Omar Chande), muigizaji bora wa kike(Godliver Gordian), 
filamu bora(AISHA) na mhariri bora wa filamu(Momose Cheyo).
Mtengenezaji huyo wa 
filamu aliyewahi kujinyakulia tuzo kadhaa kupitia filamu za SHOESHINE 
pamoja na SAMAKI MCHANGANI, akitoa ushauri kwa vijana, wasanii chipukizi
 na pia wasanii wakongwe aliwasihi wasidharau umuhimu wa kuingia 
darasani kujinoa zaidi na kupata maarifa.
Bw.Amil aliongeza,”hata
 kama chuo si chaguo la kwanza ama hauchukulii kwa uzito, kuna warsha 
nyingi sana ambazo zinasaidia kukuza kipaji na uzoefu katika 
utengenezaji wa filamu. Tafadhalini endeleni kusoma, kudadisi mambo 
mbalimbali yanayoendelea ulimwenguni, na daima ujiulize filamu zako 
zitaongelea kuhusu nini”.
Akiwashukuru wadau wa 
filamu alisiwasisitiza wajue tu kwamba Kijiweni productions ipo, na 
itaendelea kupambana na mifumo inayokandamiza na kunyanyasa watanzania 
na watu wote bila kujali rika, rangi au jinsia ya mtu.
Tamasha hilo la filamu 
huandaliwa kila mwaka na kushirikisha maonesho ya filamu na sanaa 
mbalimbali, utoaji tuzo na mafunzo kwa watengenezaji wa filamu
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni