BODI YA NHIF YAUNDA MUUNDO MPYA WA WAKURUGENZI KUTOKA WAKURUGENZI TISA HADI WATANO.
( picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii’)
………………………………………………………………………………
Na Chalila Kibbuda, Globu ya Jamii.
BODI 
ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa 
kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza 
kufanya kazi kwa kasi katika utoaji  wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza
 na waandishi habari Makao Makuu NHIF leo  Mwenyekiti bodi hiyo Spika 
Mstaafu, Anne Makinda amesema kuwa utaratibu wa awali wakurugenzi 
walikuwa wanaajiliwa kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu.
Amesema
 kuwa wakurugenzi waliokuwa wanafanya wengine kwa mikataba wengine 
wamemaliza na ambao walikuwa wanaendelea wamesitisha mikataba yao.
Makinda amesema kuwa NHIF imekaa kwa muda ikiwa haina bodi kwa mwaka mmoja na nusu hivyo baadhi ya vitu havikuwa sawa.
Amesema
 kuwa watu ambao wamemaliza mikataba na weengine kusitisha mikataba yao 
wanaweza wakaomba tena kama wana sifa ya kazi watazoomba na kuangalia 
weledi wao 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni