WAZIRI WA KILIMO DK CHARLES TIZEBA ATUMBUA MAJIPU YA TUMBAKU TABORA
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na 
Uvuvi  Injinia Dkt. Charles Tizeba amefanya ziara ya kikazi mkoani 
Tabora kwa lengo la kubaini changamoto zinazolikabili zao la tumbaku.
 Katika ziara hiyo waziri huyo  
ametembelea masoko ya zao hilo yaliyofanyika kwenye vyama vya msingi vya
 ushirika wa wakulima wa tumbaku vya Tumbi katika manispaa ya Tabora na 
Ngulu wilayani Sikonge.
 Akiwa kwenye masoko hayo ameweza
 kuzungumza na wakulima,wateuzi (classifiers) , wanunuzi 
(blenders),viongozi wa vyama vya ushirika, wajumbe wa bodi ya tumbaku 
Tanzania (TTB).
 Akifanya majumuhisho ya ziara 
hiyo mbele ya wadau wa zao hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya 
mkuu wa mkoa wa Tabora *Dkt Tizeba ameagiza yafuatayo:-*
 Makampuni yanayonunua  tumbaku mkoani Tabora kuwalipa wakulima malipo yao ya pili bila masharti ya miti.
 Bodi ya Tumbaku kufanya hesabu 
ya kilo zilizokuwa zikikatwa na makampuni yanayonunua zao hilo kwa kile 
kinachodaiwa “mnyauko” ambao unaosababisha uzito wa tumbaku kupungua kwa
 kuwa mnunuzi amechelewa kuondoa Tumbaku yake kwenye Magodauni baada ya 
kuinunua, baada ya hesabu hiyo makampuni yatawalipa wakulima kwa msimu 
huu na misimu mingine iliyopita.
 Mabenki yote yaandike mikataba yote kwa lugha ya Kiswahili ili wakulima waweze kuielewa mikataba hiyo.
 Mabenki kuacha kuwaibiwa 
wakulima kwa kucheza na ubadilishaji fedha kutoka dola ya kimarekani 
kwenda kwenye shilingi ya Tanzania.
 Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB kuhamisha makao yake makuu kutoka Morogoro hadi mjini Tabora.
 Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB 
kuacha kuburuzwa na makampuni yanayonunua Tumbaku au Tobacco Council na 
badala yake wasimamie sheria kikamilifu.
 Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB 
kuanzia msimu ujao wa masoko ifute kabisa matumizi ya mizani ya rula na 
aina zake zote na badala yake itumike mizani ya electronic ili kuandoa 
wizi kupitia mizani.
 Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB ipunguze madaraja ya Tumbaku kutoka 72 ya sasa.
 Mabenki kuacha kuyaingiza makampuni ya ununuzi wa Tumbaku kwenye mikataba ya mikopo kwenye vyama vya msingi.
 Mrajis wa vyama vya Ushirika 
nchini kuhakikisha vyama vya msingi ahakikishe vyama vya Ushirika 105 
kati ya 217 vilivyoko hatarini kufutwa mkoani Tabora vinarejea kutoa 
huduma kwa wanachama wao badala ya kuvifuta.
 Mrajis atapoteza ajira yake ikibainika chama cha Ushirika au SACCOS imekufa.
 Kuanzia msimu ujao Chama Kikuu 
Cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi WETCU LTD hakita endeshwa na 
fedha ya makato ya moja kwa moja kutoka kwenye kila kilo ya tumbaku na 
badala yake wataomba fedha kutoka vyama vya msingi ambavyo ni mwanachama
 wa WETCU LTD na sio mkulima mmoja mmoja.
 Halmashauri ya Tumbaku (Tobacco Council) sio chombo cha kisheria hivyo kisitumike kumkandamiza mkulima.
 Mkulima hatokatwa kilo moja (mara mbili) kwa ajili ya uzito wa gunia analofungia tumbaku.
 Ni mara ya kwanza na ya mwisho 
kwa mtendaji mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania kushindwa kufika kwenye 
ziara ya waziri mwenye dhamana.
 Independent Famers (IF) na Association ni marufuku kwa kuwa zilitumika kuua ushirika.
 Wakulima waache kuchanganya grade tofauti za tumbaku kwenye mtumba mmoja.
 Wakulima wadhibitiwe kutorosha tumbaku.
 Kwenye vyama vya Msingi akopeshwe mkulima mmoja mmoja na sio kwa vikundi ili kila mmoja abebe mzigo wa kulipa deni lake.
 Waziri Tizeba amebaini yafuatayo katika ziara hiyo:-
 Uchaguzi wa viongozi kwenye vyama vya Ushirika ni Vita kuliko hata kugombea Ubunge.
 Tumbaku haijabadilisha maisha ya watu.
 Asilimia 90 ya matatizo yaliyoko
 kwenye vyama vya msingi vya ushirika yamesababishwa na watu walioko nje
 ya vyama hivyo na asilimia 10 ni wanachama wa vyama hivyo.
 Kwenye masoko wanunuzi (Blenders) wanasauti kuliko wateuzi wa serikali (classifiers).
 Maofisa ushirika ni chanzo cha kufa kwa vyama vya Ushirika.
 Mrajis ni chanzo cha kufa kwa vyama vya ushirika kwa kuwa anaidhinisha mikopo, utoaji fedha,bajeti na nk.
 Mabenki ni chanzo cha kufa kwa vyama vya ushirika yanatumia uelewa mdogo wa wakulima kujinufaisha kwa wizi.
 Bodi ya Tumbaku Tanzania TTB ni chanzo cha kuua ushirika kwa kuwa imeshindwa kutimiza wajibu wake.
 Tobacco Council inaamua kila kitu na sio Bodi ya Tumbaku Tanzania.
 Viongozi wa vyama vya msingi wanaingia mikataba wasiyoijua au kuielewa.
 Mikopo ya mabenki imekatiwa bima lakini vyama vya msingi vikishindwa kulipa mikopo hiyo bado wanaendelea kudaiwa.
 Zabuni za usambazaji Pembejeo zinatolewa kwa misingi ya Rushwa.
 Bei ya mbolea inayonunuliwa kwa jumla ni kubwa kuliko bei ya rejareja.
 Kwenye soko kuna madaraja 72 ya 
tumbaku ambapo tumbaku hiyo hiyo ikifika kiwandani Morogoro kuna kitu 
kinaitwa “inhouse grading” inayotoa madaraja zaida ya 100 yasiyohusiana 
na madaraka yanayotumika kwenye soko.
 Mabenki yamevikopesha Vyama vya 
msingi AMCOS ili vijenge Maghala huku wakandarasi wakiwekwa na Mabenki 
hayo hayo baadhi ya Maghala hayajakamilika na Mabenki yanaendelea kukata
 fedha za Wakulima kulipa mkopo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni