KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
WAKATI
wasanii wa kundi la ngoma za utamaduni la Utandawazi wanajipanga
kutumbuiza, watu wengi waliokusanyika kwenye viwanja wa shule ya msingi
Bukongo mjini Nansio walikuwa wanajiuliza mtoto Gozbert Bwele (8)
aliyekuwa amekumbatia ngoma alikwenda kufanya nini pale.
Lakini
mara tu ngoma zilipoanza kupigwa, uwanja mzima ukalipuka kwa furaha na
haikushangaza wakati makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria
Teresa Fernandez de la Vega, aliposhindwa kuvumilia na kutoka kwenda
kucheza na mtoto huyo aliyeonyesha
ufundi mkubwa katika upigaji wa ngoma. Mama Maria Teresa, ambaye ni rais wa taasisi ya Mfuko wa kusaidia Wanawake Afrika, alijitoma uwanjani kucheza na kumtunza mtoto huyo anayesoma darasa la kwanza kwenye shule ya msingi Nansole katika halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

Makamu
huyo wa Rais mstaafu wa Hispania alizuru kisiwani Ukerewe akiwa
ameongozana na ujumbe wake kwa lengo la kujionea kilimo cha viazi lishe
na usindikaji wa mazao mbalimbali yatokanayo na viazi hivyo. Kilimo
hicho kinafanywa na akinamama 25 chini ya Mradi wa Green Voices
unaofadhiliwa na taasisi ya Mfuko wa kusaidia Wanawake Afrika, ambao kwa
hapa nchini umewawezesha wanawake wa Tanzania kubuni miradi endelevu
inayoendana na utunzaji wa mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko
ya tabianchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni