| Wanafunzi wa  shule  ya msingi Mihayo waakifurahia madawati mara baada ya makabidhiano hapo shuleni 
 
 
Julai 18 2016 Tabora:
 Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 350 yenye thamani ya
 shilingi milioni 58 kwa shule 12 za msingi katika wilaya ya 
Tabora(50),Nzega(200) na Urambo(100) ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo 
katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika 
shule za msingi nchini. 
Akizungumza
 leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi 
Mwangoye katika manispaa ya Tabora, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa 
Ally Maswanya amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya
 kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo 
nchini.  
“Mchango
 huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika 
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini 
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga 
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo 
madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Maswanya. 
Maswanya
 amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika 
shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dar 
es Salaam, Mwanga  na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa 
madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo. 
Makabidhiano
 yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora mheshimiwa Aggrey Mwanri ambaye
 alisema madawati hayo 350 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa 
watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga 
mkono zoezi hilo. 
“Tunapenda
 kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu 
kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la 
ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa 
Tabora. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 350 yatawawezesha mamia
 ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao 
katika mazingira bora zaidi,” alisema Mwanri. 
Madawati
 hayo 350 yametolewa Tabora kwa shule za msingi 12 kama ifuatavo, 
Mihayo,Kasela,Shigamba,Itobo,Mwamala,Mwangoye,Umoja,Urambo,Ukombozi,Ussoke,
 Tulieni na Mabatini.  | 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni