MAN UTD DORTMUND KUFUNGUA PAZIA LA MICHUANO YA ICC ITAKAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES
Na Dotto Mwaibale
IKIWA
chini ya kocha wake mpya Mreno, Jose Mourinho, Manchester United
wanatarajia kushuka dimbani jijini Shanghai, China kuwakabili Borrusia
Dortmund siku ya Ijumaa Julai 22, 2016 mechi itakayopigwa saa tisa za
alasiri kwa saa za hapa nyumbani kupitia ving’amuzi vya StarTimes.
Akizungumzia
juu ya habari hiyo njema kwa wapenda soka nchini Makamu wa Rais wa
StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa michuano hiyo
itakuwa ni ya kusisimua kutokana na orodha ndefu ya timu kubwa
zitakazoshiriki kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United,
Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus, Liverpool, Chelsea na
Bayern Munich kwa uchache.
“Tunayofuraha
kuwatangazia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa watapata fursa
ya kutazama timu zao katika mechi za awali kabla ya kuanza kwa ligi kuu
mbalimbali duniani kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee. Mechi zote za
michuano ya ICC itaonekana moja kwa moja kupitia chaneli ya World
Football inayopatikana katika kifurushi cha Mambo kwa malipo ya shilingi
12000/- tu kwa mwezi. Michezo yote itakuwa ni yenye msisimko mkubwa
kwani timu zinazoshiriki ni kubwa, nyingi zikiwa ni mabingwa katika ligi
kuu zao, zina wachezaji nyota na kikubwa zaidi zingine hazikuwahi
kukutana kabla.” Alisema Bi. Hanif
“Hii
ni fursa ya pekee kwa watanzania kwani tunafahamu ya kuwa ni wapenzi
wakubwa wa mchezo huu na siku zote StarTimes tunajitahidi kuwapatia kile
wanachokipenda. Hii ni mara ya pili tunaonyesha moja kwa moja michuano
hii kwani mwaka jana tulifanya hivyo ambapo timu ya Real Madrid
waliibuka mabingwa. Hivyo basi mashabiki watakuwa na shauku kubwa ya
kujua ni timu gani itakayoibuka mabingwa au kama utarudi kwa Real
Madrid,” alisema na kumalizia Bi. Hanif kuwa, “Ni wajibu wetu
kuhakikisha wanafikiwa na matangazo ya vipindi vizuri na kusisimua kama
hivi kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu ambazo kila mtu
atazimudu.”
Mchezo
huo ni sehemu ya ufunguzi wa michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa
almaarufu kama International Champions Cup au ICC itakayoanza kutimua
vumbi Julai 22 na kumalizika Agosti 13, 2016 katika viwanja mbalimbali
nchini Marekani, Ulaya, Australia na China.
Katika
michuano hii wapenzi wa soka duniani watapat fursa kujionea kwa mara
kwanza mechi ya watani wa jadi kutoka jiji la Manchester au
unavyojulikana kama ‘Machester Derby’ miongoni mwa mashabiki wengi.
Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatatu ya Julai 25 jijini Beijing, China.
Mchezo
huo utanogeshwa si tu na ushindani baina ya wachezaji au mashabiki bali
safari hii ni makocha waliopewa vibarua vya kunoa vikosi hivyo, Jose
Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.
Ukiachana
na mechi hiyo, pia macho ya mashabiki wengi yatakuwa yakisubiria kwa
hamu kutazama mechi kali zitakazozikutanisha timu za, Real Madrid na
PSG, Chelsea na Liverpool, Real Madrid na Chelsea, Bayern Munich na
Real Madrid pamoja na Liverpool na Barcelona.
Kwa
ujumla timu zitazoshiriki michuano hii ni pamoja na Real Madrid,
Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain
(PSG), Juventus, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham
Hotspurs, AC Millan, Inter Millan, Leicester City FC, Celtic FC,
Atletico Madrid, Melbourne Victoria na South China.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni