JB, Mataluma, Kitime ndani ya igizo ya kuhamasisha Kilimo
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Msanii
 nyota nchini wa filamu, Jacob ‘JB’ Steven ni miongoni mwa waigizaji  
mbalimbali walioshiriki katika igizo la  Kumekucha ambayo imeandaliwa 
kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujishughulisha na kilimo kutokana na 
uhaba wa soko la ajira.
Igizo
 hilo ambali pia ni mchezo wa redio (radio plays) limeandaliwa na 
taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development 
International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la 
Maendeleo (Usaid) ya ushauri wa Taasisi ya chakula na lishe (TFNC), 
Taasisi ya TAHA, ACDI VOCA – NAFAKA,  Land O Lakes, Rudi, Mwanzo Bora, 
The Rice Council of Tanzania, Technoserve, ANSAF (Non State Action 
Forum) na taasisi ya AMSHA.
Katika
 filamu hiyo, JB anatumia jina la Mzee Kidevu ambaye kazi yake kubwa ni 
kununua mazao kwa wakulima kwa bei ya ukandamizaji na kuwafanya wakulima
 hao kuendelea kuwa na maisha duni huku yeye akijinufaisha.
Akizungumza
 katika uzinduzi huo, JB alisema kuwa amefurahi sana kushiriki katika 
filamu hiyo ambayo inafundisha na kuhamasisha vijana kujihusisha zaidi 
na masuala ya kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini kama suluhisho
 lao la kutatua matatizo yao.
“Nimepanda
 kushiriki katika filamu na mchezo huu wa redio, umenipa mwanga mkubwa 
na kupanua wigo wa kazi yangu ya kuigiza, kabla ya kuingia kwenye 
kuigiza, nilikuwa mnunuzi wa mazao hasa mahindi kule Kibaigwa na kusaga 
na kuuza unga wa chakula, hii ilikuwa fursa kwangu na nimeipenda, 
nawashukuru wahusika wote waliofanikisha filamu hii,” alisema JB.
Mkurugenzi
 wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester alisema kuwa wamefurahi 
kujihusisha na masuala mbalimbali yaa maendeleo hapa nchini na kuamua 
kusaidia mradi huo ambao unahusika zaidi  maeneo ya  vijini.
“USAID
 imejihusisha katika miradi mingi ya maendeleo nchini, kama unajua, 
zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanajihusisha na masuala ya kilimo, 
waahitaji kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa ya maendeleo, mchezo wa 
Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” alisema Chester.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni