Serikali yafanya mazungumzo na Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu nchini.
………………………………………………………………………………………….
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Serikali
 imekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho 
ya Filamu nchini ikiwa ni sehemu ya kubaini changamoto mbalimbali 
zinazoyakabili Mashirikisho hayo.
Akiongea
 hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo
 ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah 
Kihimbi alisema kwamba, Mashirikisho yanayounda Shirikisho la Filamu 
nchini hayanabudi kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kubaini 
changamoto na namna ya kuzitatua kwa manufaa ya Wasanii na Taifa kwa 
ujumla.
Alieeleza
 kuwa, Wasanii wanapaswa kuzingatia maadili wakati wanapofanya kazi zao 
za sanaa ili waweze kujijengea heshima kwao, kwa jamii ambayo ndio mlaji
 wa kazi zao za kisanaa na kwa Taifa kwa ujumla.
“Mnapofanya
 kazi zenu za sanaa, jitahidini kufuata miiko ya kazi zenu, tumieni 
vipaji vyenu vizuri kwa kufuata maadili ya Kitanzania, lakini pia 
jitahidini kuwainua wale wasanii wanaochipukia ama wale wadogo ili 
waweze kuwa na hamasa ya kuendeleza kazi zao za sanaa”, alisema, Bi. 
Kihimbi.
Bi. 
Kihimbi aligusia suala la fursa ya kazi za sanaa inayodhaminiwa na 
Taasisi ya British Council Tanzania na kuwataka wasanii kuchangamkia 
fursa hiyo kwa kuhakikisha kuwa kila msanii au kikundi kinaandika 
Pendekezo (Proposal) kuhusu fursa hiyo ili kujiwekea nafasi 
kubwa kwa wasanii wa Tanzania kushinda fursa hiyo na kuweza kupata fedha
 za kuendesha kazi za sanaa kulingana na wazo lililobuniwa.
“Kuweni wabunifu katika hii fursa ili mje na wazo zuri ambalo litawawezesha kushinda hii fursa hasa hii ya nAnA (new Arts new Audiences) kwani inamhusu msanii mmoja mmoja au kikundi”, alisema, Bi. Kihimbi.
Aliongeza
 kuwa, Serikali itajitahidi kutatua baadhi ya changamoto ambazo 
zinaonekana kuwa kero kwa wasanii nchini ikiwemo suala la wizi wa kazi 
za sanaa (Piracy) ambalo kwa sasa tayari Waziri mwenye dhamana 
katika Wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye ameonyesha mfano kwa kukamata DVDs 
feki pamoja na mitambo ikiyotumika kudurufu kazi hizo za sanaa nchini.
Kwa 
upande wake, Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alisema
 kwamba Bodi yake inashirikiana vema na wasanii nchini kwa kuzingatia 
Sheria za nchi pasipo kumuonea msanii yeyote na kuwataka wasanii kote 
kuendeleza uhusiano huo mzuri uliopo kwa manufaa yao na Taifa kwa 
ujumla.
Aidha,
 aliwataka viongozi wa Shirikisho hilo la Sanaa kuendelea na utaratibu 
wa kupeana taarifa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sanaa na 
kuwahimiza wasanii kupenda kujiendeleza kielimu ili waweze kumudu soko 
huku akiwasisitiza kuhakikisha kuwa kazi zao wanazotengeneza zinapata 
kibali cha Bodi kwa kuwekewa madaraja na zinakuwa na stika halali ya 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuepusha uharamia wa kazi zao.
Naye 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Simon Mwakifwamba ameiomba 
Serikali kuendelea kushirikiana na Wasanii kwa karibu kwa kuzifanyia 
kazi baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo na ikiwemo suala la 
uharakishaji wa Sera ya Filamu kwani ndiyo kipaumbele chao cha kwanza, 
elimu ya namna ya kutengeneza filamu bora, usambazaji wa kazi zao pamoja
 na adui yao mkubwa ambaye ni uharamia wa kazi za sanaa.
Ameishukuru
 Serikali kwa kuunda Sekta mpya ya Sanaa na kusema kuwa, Sekta hiyo 
itakuwa Mkombozi kwao kwani wanajisikia fahari kutambuliwa na kuwa na 
kitengo chao cha masuala ya kazi zao huku akiaahidi ushirikiano mzuri 
kwa sekta hiyo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni