TAARIFA YA UTEUZI WA VIONGOZI KATIKA TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. 
Abdulhamid Y. Mzee, katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la 
Mapinduzi Dkt. Juma Yakout Juma ametuliwa kuwa Naibu Katibu Msaidizi 
Baraza la Mapinduzi (Sera, Ufuatiliaji na Tathmini).
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ameteuliwa Nd. Mwadini Makame Haji.
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, 
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti 
Nd. Abdalla Issa Mgongo na Mkurugenzi wa Miundo ya Taasisi, Utumishi na 
Maslahi ya Watumishi Nd. Shaibu Ally Mwazema.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, 
Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa 
na Serikali za Mitaa Nd. Khalid Omar Abdalla na Katibu wa Tawala wa 
Wilaya ya Magharibi ‘A’ Nd. Mashaka Hassan Mwita.
Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa
 Rais Nd. Issa Mlingoti Ally ameteuliwa kuwa Mratibu Mkuu wa Ofisi ya 
Uratibu wa Shughuli za SMZ, Dar es  salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Nd. AMEIR Makame Ussi
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa
 shughuli za Serikali Nd. Khalid Bakari Amran, Mkurugenzi wa Idara ya 
sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Nd. Riziki Daniel Yussuf na Ofisa 
Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba Nd. Ali Salim Alim 
Matta.
Wizara ya Afya Mkurugenzi wa 
Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Nd. Ramadhan Khamis Juma na Ofisa 
Mdhamini wa Wizara ya Afya  Pemba Nd. Ali Bakari Ali.
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na UvuviMkurugenzi wa Umwagiliaji Maji Nd. Haji Hamid Saleh.
Wizara ya Habari, Utalii, 
Utamaduni na Michezo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa na Sensa ya 
Filamu na Utamaduni Dkt. Omar Abdalla Adam.
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na 
Usafirishaji Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Nd. Abdalla A. 
Mwinyigogo na Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Nd. Ramadhan Mussa Bakari.
Katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Omar Ali Omar Bhai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
Wizara ya Ardhi, Mji, Nishati na 
Mazingira Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Tahir M. K. Abdalla na 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Maji na Nishati 
(ZURA) Nd. Hemed Salim Hemed.
WIZARA YA Biashara Viwanda na Masoko Mkurugenzi wa Mipango, sera na Utafiti Nd. Nana Mwanjisi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni