Mwanariadha
wa zamani aliyewahi kushika nafasi ya pili duniani katika mashindao ya
Olimpiki nchini Ugiriki Bw. John Stephen Akhwari (wa kwanza kulia)
akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo
Mhe.Anastazia Wambura (katikati) Mwenge aliyoukimbiza katika viwanjani
vya Beijing nchini China wakati wa kufungua mashindano ya Olimpiki mwaka
2008 alipomtembelea nyumbani kwake katika Kijiji cha Khaday, Kata ya
Sanu Mjini Mbulu,(wakwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu
Bw.Chelestino Mofuga.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura
(katikati) akiwa ameshikilia kikombe cha ushindi wa Mwanariadha wa
zamani John Stephen Akhwari alichoshinda shinda katika Mashindano yaya
Olimpiki yaliyofanyika nchini Ugiriki kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Mbulu Bw.Chelestino Mofuga (wa kwanza kushoto) na John Steven Akhwari
mwenye (wa kwanza kulia) wakiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Khaday,
Kata ya Sanu.
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura
akisalimiana na Daktari wa Timu ya Jeshi la Wananchi Andrew Panga leo
alipotembelea timu hiyo kambini Mjini Mbulu akiwa katika ziara ya
kikazi (wakwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia
Wambura(wasita kulia) akiwa katika picha ya pamoja leo na Timu ya
wanariadha wa Jeshi la Wananchi waliyoko kambini Wilayani Mbulu
alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi (wasita kushoto) ni
mwanariadha wa zamani John Stephen Akhwari pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.
Mwanariadha
wa zamani aliyeweka rekodi ya Kimataifa ya kuonyesha Uzalendo kwa nchi
yake katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Mexico mwaka 1968 kwa
kuendelea kukimbia na kushika namba mbili mbali na kwamba alikuwa
amevunjika mguu wakati akiwa uwanjani Bw.John Stephen Akhwari akileza
changamoto za sekta ya riadha nchini katika Mkutano wa wadau wa kisekta
na Naibu Waziri Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura
(hayupo pichani) ulifofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara.
Mwanariadha
wa zamani aliyeiletea Tanzania sifa kwa kushinda mashindano mbalimbali
ya Kimataifa na kupata Medali za aina mbalimbali Bw.Alfredo Shahanga
akieleza changamoto zilizojitokeza wakati wadau wa kutoka nchini
Australia walipokuja Tanzania na kutaka kujenga uwanja wa michezo
Wilayani Mbulu kumuenzi mwanariadha mzalendo John Stephen Akhwari kwa
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura
(hayupo pichani) leo katika mkutano wa wadau wa kisekta Mkoani Manyara.
Na Anitha Jonas- MAELEZO,BABATI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni