NITAHAMIA DODOMA SEPTEMBA MWAKA HUU – WAZIRI MKUU
…………………………………………………………………………………………………………………..
*Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja
WAZIRI MKUU 
Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu 
kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa 
wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
“Jana 
nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe 
matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma 
ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa 
Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.
Amesema tangu 
Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na 
wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa
 ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. 
John Magufuli.
“Wananchi kazi
 mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa 
mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja 
Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati 
wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji 
wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.
Amewataka 
wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha 
umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi 
za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu 
watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.
Wakati huo huo,
 mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza
 nia ya Serikali kuhamia  Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili 
kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage 
Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.
Akizungumza na
 mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku 
akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao 
makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya 
kwnza ya uongozi wake.
“Kama wabunge 
karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa
 miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama 
kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali 
ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.
Mara kwanza 
kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati 
akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti 
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.
Rais Magufuli 
amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani 
iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi 
mashujaa walioipigania nchi hii.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni