MKAZI WA MLANDIZI KIBAHA PWANI APATA UPOFU BAADA YA KUMEZA DAWA AINA YA FANSIDER AOMBA MSAADA ML.18
(PICHA NA VICTOR MASANGU).
……………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI  
MKAZI
 mmoja ajulikanaye kwa jina la Seleman Mgoto (42)anayeishi katika 
kitongoji cha Janga kilichopo eneo la Mlandizi  Wilayani Kibaha Mkoa wa 
Pwani ameathirika macho yake mawili na kupoteza kabisa uwezo wa kuona 
 baada ya kutumia dawa ya kutibu malaria  aina ya Fansider  hivyo 
anahitaji msaada wa kiasi cha shilingi milioni 18 kwa ajili ya kwenda 
kupatiwa matibabu zaidi  nchini India.
Hayo
 yamebainika baada ya mwandishi habari hizi  kuweza kufika nyumbani  kwa
 kaka yake maeneo ya mlandizi ambapo ndipo anapoishi kwa sasa baada ya 
kupatwa na tatizo hilo na kuweza kuzungumza naye kuhusiana na mkasa wa 
tukio hilo lililompata.
Akizunguza
 kwa  masikitiko makubwa  Mgoto alisema kwamba mnano  agosti  2012 
alikuwa anaumwa  na alipokwenda kupimwa aligundulika kuwa na wadudu 
tisa  wa ugonjwa wa malaria ndipo alipoandika dawa aina ya fansider na 
kuamua kwenda kuzinunua katika moja la duka la madawa lililopo maeneo 
hayo ya mlandizi na baada ya kuzimeza hali yake baada ya siku mbili 
ilianza kubadilika kutokana na sumu  kali iliyokuwepo mwilini mwake  .
“Mimi
 mwezi agosti mwaka 2012 ndugu zangu waandishi niliweza kuumwa na 
nilipoenda kupima afya niligundulika nina malaria, na baada ya hapo 
niliweza kuandikiwa dawa na nikaenda kununua dawa aina ya fansider, ila 
baada ya siku mbii hali yangu iiweza kubadilika na nilipokwenda kituo 
cha afya niilazwa kwa ajili matibabu zaidi,”alisema.
Aidha
 akifafanua kuhusina na kuangaika katika hospitali mbali mbali kwa ajili
 ya matibabu alisema kwamba mara ya mwisho alikwenda kuwaona madaktari 
bingwa wa hospitari ya CCBRT ya jijini Dar es salaam ambapo walimwambia 
macho yake kwa hapa Tanzania hayawezi kutibiwa mpaka aende nchini India 
ndio yanaweza kupona.
Pia
 katika hatua nyingine amesema kwamba kwa sasa maisha yake yamekuwa ni 
magumu sana kutokana na kutokuwa na kipato chochote kile anachokiingiza 
ukizingatia ana familia mke pamoja na watoto watatu ambao wanamtegemea 
kwa kila kitu ambapo watoto wengine  wawili wapo wanasoma sekondari 
hivyo kunahitajika mahitaji mengine ya msingi.
Mwenyekiti
 wa kamati maalumu ya kumsaidia  kwenda kupatiwa matibabu nchini India 
Eria Chaofu pamoja na Luiza Mdachi ambaye ni dada  yake  wamesema kwamba
 familia   imeangaika kwa hali na mali  kwa kipindi cha miaka mitatu 
katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya  kumtibia bila ya kupata 
mafanikio yoyote kutokana  na kutokuwa na uwezo wa kifedha. miaka mitatu
  
Aidha
 Mwenyekiti huyo amemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Mgufuli 
kumsaidia mgonjwa huyo pamoja na wadau wengine wakiwemo wakuu wa wilaya,
 wabunge, wakuu wa miko pamoja na Wizara ya afya ili aweze kwenda 
kutibiwa na kurudi katika hali.
 Kwa 
 mtu yoyote ambaye ameguswa na anahitaji kumsaidia mchango wake  kwa 
hali na mali  Seleman Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa wa 
macho yake mawili,atume  kwa tigo pesa –0655-413939 au M-PESA 0754-413939 na akaunti namba NMB -80110000915 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini India kwani zinahitajika shilingi milioni 18.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni