TBL Group yadhamini semina ya wakaguzi wa magari wa polisi Mwanza
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu-Mwanza
Katika
mkakati wake wa kushirikiana na serikali na jamii katika kutoa elimu
ya usalama,kampuni ya TBL Group imedhamini semina kwa wakaguzi wa
magari kutoka Jeshi la Polisi jijini Mwanza ambayo imefanyika katika
kiwanda cha TBL cha Mwanza na kuendeshwa na Mtaalamu wa magari kutoka
kampuni ya CFAO,Bw.Hubert Kubo.
Semina
hiyo iliendeshwa kwa njia shirikishi ambapo washiriki walijadiliana
masuala mbalimbali yanayohusiana na usalama barabarani na changamoto
zilizopo katika kukagua vyombo vya moto na jinsi ya kupunguza ajali za
barabarani nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni