BFA YAPATA VIONGOZI WAPYA WA MIAKA MINNE IJAYO
………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
CHAMA
cha mpira wa miguu ,wilayani Bagamoyo,mkoa wa Pwani,( BFA) kimechagua
viongozi wapya wa chama hicho wataokingoza katika kipindi cha miaka
minne .
Uchaguzi huo umefanyika kihalali ,kwa mujibu wa sheria ambao ulihudhuliwa na wajumbe 91.
Katika
uchaguzi huo alhaj AbdulZahoro Sharifu alichaguliwa kuwa mwenyekiti kwa
kipindi kitakachoishia mwaka 2020 kwa kupata kura 77.
Alhaj
Sharif alipata ushindi huo kwa kupata kura hizo dhidi ya mpinzani wake
Kitomu Yona aliyepata kura 11 huku nafasi ya makamu mwenyekiti
alichaguliwa Shaabani Makelele ambae hakuwa na mpinzani.
Nafasi
ya katibu mkuu imenyakuliwa na John Fransis Bolizozo “Boli Kubwa”
aliyejipatia kura 81 na kumwacha mbali mgombea mwenzie kwenye nafasi
hiyo Yona Mkawa aliyejinyakulia kura 4.
Katibu
msaidizi alishinda Jitihada Omary kwa kura zote kutokana na kuwa peke
yake ,mhazini alichaguliwa Ornjurie Marigwa ambae hakuwa na mpinzani
msaidizi ikienda kwa Salumu Kanuti aliyejikusanyia kura 88.
Mjumbe
mkutano mkuu wa mkoa alichaguliwa kipa wa zamani wa nyota nyekundu na
kocha mzawa hapa nchini Shekhe Abdallah aliyepata kura 45 dhidi ya kura
43 alizopata Mzee Minjoli.
Nafasi
ya mwakilishi wa vilabu akichaguliwa Jabir Omary aliyeshinda kwa kura
46 akimwacha mgombea mwenzake Ally Jakaya aliyepata kura 44.
Wajumbe
kamati ya utendaji na kura zao katika mabano waliochaguliwa ni
Ramadhani Mape (77), Rajabu Maliki (80), Maneno Kidobe (68), Shabani
Masimbi (69) na Peter Nyambasi (39).
Katika
uchaguzi huo uliongozwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wilaya
Mwinyi Akida, mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shaabani Kangale
“Machokodo” na diwani wa kata ya Kiwangwa Hussein Malota Kwaga.
Baada
ya kutangaza matokeo hayo Akida aliwataka viongozi hao kuhakikisha
wanawatumikia ipasavyo wana-Bagamoyo ili mpira uchezwe maeneo yote.
Alieleza
kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kukidhi kiu ya wana michezo ambao kwa
muda mrefu hususan ukanda wa Chalinze na maeneo mengine wilayani humo
ambao wamekosa fursa hiyo.
Nae
mwenyekiti mpya wa BFA ,Abdul Sharif, alitoa rai kwa viongozi wengine
wa chama hicho kuhakikisha kila mmoja anajitoa kwa hali na mali ili
kuinua sekta ya michezo wilayani humo.
Alhaj
Sharif aliahidi kupatikana kwa timu itakayocheza ligi kuu ya Vodacom
Tanzania Bara katika kipindi cha miaka minne ambacho watakiongoza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni