Balozi
Ombeni Sefue akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Utafiti
wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati
alipofanya ziara katika taasisi hiyo mwishoni mwa wiki ili kujionea
shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi hiyo , Kwa kiwango
kikubwa (NHBRA) imeonyesha ni taasisi inayoweza kujenga nyumba za bei
nafuu sana hasa vijijini ili watanzania wa maeneo hayo waweze kupata
makazi bora ya kuishi kwa bei rahisi zaidi, Kulia katika picha ni
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi.
Taasisi hiyo pia imekuwa
ikijihusisha na mafunzo teknolojia ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu
kwa vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuwafundisha juu ya
utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba pamoja na ujenzi wa
nyumba za zenyewe ambapo taasisi na wananchi mbalimbali wanaweza
kufaidika na mpango huo nchini.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES
SALAAM)
Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi akizungmza wakati
alipokuwa akimkaribisha Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea katika
taasisi ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi
NHBRA Mwenge jijini Dar es salaam.
Bw.
Sylivester Shumbusho Fundi kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba
na Vifaa vya Ujenzi NHBRA akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue juu ya
utengenezaji wa matofali ya bei rahisi kwa kutumia udongo wakati
alipokuwa akitembelea karakana ya taasisi hiyo iliyopo Mwenge jijini Dar
es salaamKatikati ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson
Mturi.
Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi akimpa maelezo Balozi Ombeni
Sefue wakati alipokuwa akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali katika
taasisi hiyo kulia ni Bw. Sylvester Shumbusho Fundi katika taasisi
hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kutengeneza vigae vya kuezekea nyumba katika karakana ya taasisi hiyo.
Balozi Ombeni Sefue akitembezwa
na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiku Samson Mturi maeneo mbalimbali
ili kujionea shughuli za zinazofanywa na taasisi hiyo.
Balozi
Ombeni Sefua akishiriki katika shughuli ya kufyatua matofali kazi
inayofanywa pia na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali
vya ujasiriamali nchini kote.
Balozi
Ombeni Sefua akiangalia kazi ya kufyatua matofali inayofanywa pia na
Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali
nchini kote.
Balozi Ombeni Sefue akiangalia wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wakitengeneza vigae kwa ajili ya kuezekea nyumba.
Balozi Ombeni Sefue akipiga picha
kwa simu yake huku wafanyakazi wa taasisi hiyo wakimuangalia baada ya
moja ya nyumba ndogo iliyojengwa katika ghala ya taasisi hiyo kwa ajili
ya mfano kumfurahisha.
Balozi
Ombeni Sefue pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson
Mturi wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo mara baada
ya kukamilika kwa ziara hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni