RAIS DKT. ALI MOHAMED SHEIN AMEFANYA UTEUZI WA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI ZA SERIKALI.
Rais
 wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Ali Mohamed
 Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi imeeleza kuwa
- BODI YA MAPATO (ZRB)
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 14 cha sheria ya Bodi ya 
Mapato  ya 1996, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi 
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Amour Hamil Bakar kuwa 
Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar. Bwana Amour Hamil Bakar anachukua 
nafasi ya Bwana Abdi Khamis Faki ambae anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Utezi huo unaanza tarehe 1 Agost 2016.
Aidha
 kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 15(1) (A) cha sheria hiyo
 kama ilivyorekebishwa na kifungu 11 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2000, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali 
Mohamed Shein amemteua Bibi Khadija Shamte Mzee kuwa Naibu Kamishna wa 
Bodi ya Mapato ya Zanzibar. Bibi Khadija Shamte Mzee anachukua nafasi ya
 Bwana Hafidh Ussi Haji ambae uteuzi wake umefutwa.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
2.TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Tume ya 
Maadili ya Umma Namba 4 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa 
baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Said 
Bakari Jecha na Bibi Sebtuu Mohammed Nassor kuwa Makamishna wa Tume ya 
Maadili ya Viongozi wa Umma.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai, 2016.
- BODI YA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 11(1)(a) cha Sheria ya 
Shirika la Magazeti  ya Serikali Namba 11 ya 2008, Rais wa Zanzibar na 
Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein 
amemteua Bibi Umi Aley kuwa Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika 
la Magazeti ya Serikali.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
- TUME YA UTANGAZAJI
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Tume ya
 Utangazaji ya Zanzibar Namba 6 ya 1997, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti 
wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dkt. Ali 
saleh Mwinyikai  kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
- BARAZA LA SANAA NA SENSA YA FILAMU NA UTAMADUNI
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya 
Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na utamaduni Namba 7 ya 2015, Rais wa
 Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed 
Shein amemteua Bibi Maryam Mohamed Hamdan kuwa mwenyekiti wa Baraza la 
Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
- BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Baraza 
la Mitihani la Zanzibar Namba 6 ya 2012, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti 
wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi 
Maryam Abdalla Yussuf kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
- SHIRIKA LA VIWANGO LA ZANZIBAR (ZBS)
Kwa 
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8(2)(a) cha Sheria ya 
Shirika la Viwango la Zanzibar Namba 1 ya 2011, Rais wa Zanzibar na 
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein 
amemteua tena Profesa Ali Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya 
Wakurugenzi ya Shirika la Viwango la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABRI MAELEZO ZANZIBAR.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni