NAIBU WAZIRI MPINA AZITAKA RADIO ZA JAMII KUHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA
……………………………………………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka
Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu Waziri
Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa,
mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Akitolea Mfano wa Radio Pride FM
ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara,
ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake
kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo
kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.
Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea
Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la
kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa
kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya
kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea
mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.
Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa
Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri
Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za
mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani
humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi
ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.
“Nimeona kuwa uchomaji moto
misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia
nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa
uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari
kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa
alisisitiza.”
Ziara ya Naibu Waziri Mpina
Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda
na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa
Masasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni