KWA HERI MPIGANAJI JOSEPH SENGA, MUNGU AIWEKE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI
Wapiga
picha wakibeba jeneza la marehemu Joseph Senga aliyekuwa mpiga picha wa
gazeti la Tanzania Daima ili kuliweka kwenye tayari kwa safari ya
kwenda Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi wanaoongoza mbele
katikati ni Rafiki yake Mkubwa Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la
Mtanzania aliyeshika Msalaba , kulia aliyeshika Shada la maua ni John
Bukuku mpigapicha na Mkurugenzi wa Blog ya Fullshangwe na kushoto
aliyeshika picha ya marehemu ni Joachim Mushi mpiga picha na Mkurugenzi
wa Mtandao wa The Habari akiwa pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mablogger
Tanzania TBN wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Sinza jijini
Dar es salaam.
Deus
Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania akiaga mwili wa marehemu
Joseph Senga na kushoto ni Mpiga Picha mkongwe Juma Dihule.
Carthubert Kajuna Mpiga Picha na Mkurugenzi wa Blogu ya Habari na Matukio akiaga mwili wa marehemu Joseph Senga.
Mpiga Picha wa Gazeti la Habari leo Robert Okanda akiaga mwili wa marememu.
Mpiga picha Muhidin Sufiani akitoa hesgima zake za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
Baadhi ya wapiga picha wakijadiliana mambo kadhaa.
Mpiga Picha wa Jambo Leo Dotto Mwaibale akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowasa akiongozana na Nape Nnauye Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
Waziri Mkuu wa Zamani Edward
Lowasa akijadiliana jambo na Nape Nnauye Waziri wa Habari , Utamaduni ,
Sanaa na Michezo wakati walipoongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa
mwanahabari Marehemu Joseph Senga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni