WAZIRI MBARAWA AITAKA SUMATRA KUDHIBITI AJALI
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Kikwetu
Mkoani Lindi Bw. Boniface Njanda (Wa kwanza Kulia) wakati alipotembelea
uwanja huo.
……………………………………………………………………………………….
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka
uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) kutoa adhabu kali kwa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji na
madereva wazembe wanaosababisha ajali za barabarani.
Ameyazungumza
hayo wakati wa ukaguzi wa utendaji kazi kwa wafanyakazi wa taasisi
zilizopo chini ya Wizara hiyo pamoja na miundondombinu ya Barabara,
Bandari, Mawasiliano na kiwanja cha ndege cha Kikwetu mkoani Lindi.
Profesa
Mbarawa amesema kuwa ongezeko la ajali zinazosababisha vifo kutokana na
uzembe wa madereva, kutofuata sheria na alama zinazowekwa barabarani
zizidhibitiwe ili kuokoa maisha ya watanzania na nguvu kazi ya Taifa.
“Nataka
kuona wamiliki wa vyombo vya usafiri na madereva wazembe wanaposabisha
ajali na kuua watu wanafutiwa leseni zao vile vile nawataka mfikirie
kwanini watanzania wengi wanaendelea kufa kwa ajali za barabarani ili
muweze kutafuta ufumbuzi wa namna ya kudhibiti ajali hizo”, amesisitiza
Prof. Mbarawa.
Katika
hatua nyingine Waziri Mbarawa amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. George Sambali kukamilisha kazi
ya kupima eneo la kiwanja cha Kikwetu ili kupata hati miliki na
kudhibiti uvamizi wa kiwanja hicho
“Kama
kiwanja hiki hakitapimwa watu watavamia eneo la kiwanja na Serikali
italazimika kuingia gharama za kulipa fidia hivyo kuchelewesha maendeleo
ya uwanja huo”, amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kutafuta fedha kwa
kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ili kuimarisha
miundombinu ya kiwanja hicho na kuongeza chachu ya maendeleo Mkoani
humo.
Naye
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kikwetu, mkoani Lindi Bw. Boniface Njanda
amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka itafanya tathmini ya
Kiwanja hicho kabla ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Waziri
Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi wa
taasisi zilizopo chini ya Wizara na kuangalia maendeleo ya utekelezaji
wa miradi katika kanda ya kusini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni