NDIKILO :ALILIA USHIRIKIANO NA WIZARA ZA VIWANDA NA ARDHI
SERIKALI
mkoani Pwani ,imeiomba serikali kupitia wizara ya viwanda,biashara na
uwekezaji na wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi kushirikiana
na mkoa huo katika kushughulikia migogoro ya ardhi hasa inayohusisha
wawekezaji na jamii.
Aidha
imeitaka wizara ya ardhi kushirikisha wadau mbalimbali wa mkoa katika
kushughulikia migogoro hiyo ili kuondoa migongano isiyo ya lazima.
Akizungumzia
juu ya kusuasua kumalizika kwa baadhi ya migogoro ya ardhi inayohusisha
makundi ya watu na wawekezaji ,mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist
Ndikilo,alisema katika migogoro ya aina hiyo pande zote zinastahili
kupewa haki.
Alisema inawapa wakati mgumu iwapo serikali ya mkoa inakuwa na maamuzi yake na wizara ya ardhi kufikia maamuzi mengine.
Mhandisi
Ndikilo,alieleza kuwa endapo ikitokea malalamiko yoyote kuhusu
wawekezaji na jamii wanashauri wizara kuhusisha wadau wengi .
“Wizara
inawapokea watu hatukatai lakini iangalie kwani kuna makundi mengine ya
watu ambao wameshaharibu mkoani hapa ambapo wizara pasipo kujua inawapa
red capet hatimae kukwamisha juhudia za kimaendeleo zinazofanywa na
serikali ya mkoa”alisema mhandisi Ndikilo.
Mkuu
huyo wa mkoa alieleza kuwa wizara ya ardhi isiwe nyepesi kukubali
kufanyia kazi malalamiko ya kuporwa ardhi ,yanayopelekwa kwao na baadhi
ya wananchi na makundi yanayovamia mashamba ama maeneo yanayomilikiwa
na wawekezaji ambao wengi wao ni wakiukwaji wa sheria.
Mhandisi
Ndikilo alisema ushahidi walionao kimkoa kutoka katika vyombo vya dola
baadhi ya wananchi na vikundi hivyo wanauza ardhi na mapato wanayopata
hayanufaishi serikali za vijiji wala halmashauri husika badala yake
wananufaisha matumbo yao.
Alisema
wamekuwa wakijipatia mamilioni ya shilingi kwa kuuza ardhi za watu
wanaomiliki kihalali na baadae serikali ikiingilia kati wanakimbilia
wizarani .
“Serikali
ya mkoa na wilaya wakiwafikisha watu hao katika vyombo husika
wanakimbilia wizara ya ardhi na kupokelewa na kukwamisha maendeleo
lakini mkoa utaendelea kuwashughulikia ili kila mmoja apate haki yake
“alisema mhandisi Ndikilo.
Hata hivyo alisema tayari alishaandika barua juu ya maombi hayo na namna mkoa ulivyojipanga kuinua sekta ya uwekezaji .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni