MKOA WA PWANI WADHAMIRIA KUWA UKANDA WA UWEKEZAJI NA VIWANDA
MKUU
 wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,amesema amedhamiria mkoa huo
 kuwa ukanda wa viwanda na uwekezaji  ambapo hadi sasa umetenga maeneo 
yenye hekta 19,600 na hekari 3,266 kwa ajili ya uwekezaji.
Aidha
 mkoa huo tayari una viwanda 88 ambavyo ni vikubwa ,vya kati na vidogo 
huku miradi 10 ya kimkakati ipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi. 
Akizungumza
 na mwandishi wa habari hizi,mwishoni mwa wiki iliyopita ,kuhusu hali ya
 uwekezaji kimkoa,mhandisi Ndikilo ,alisema atavalia njuga suala la 
uwekezaji ili kuhakikisha mkoa unapiga hatua kiuchumi baada ya miaka 
mitano.
Alieleza
 kuwa kati ya viwanda 88 vilivyopo mkoani hapo ni pamoja na wilaya ya 
Mkuranga na viwanda  41,Chalinze 24,Kibaha mji 10,Bagamoyo viwanda 
 9,wilaya ya Kisarawe viwili na Mafia 2 viwili.
Mhandisi
 Ndikilo ,aliainisha maeneo yaliyotengwa katika halmashauri mbalimbali 
za mkoa ambapo alisema Mji wa Kibaha umetenga hekta 1,450 katika maeneo 
ya Zegereni,Misugusugu na Mtakuja .
Alisema
 eneo hilo litakuwa kwa ajili ya viwanda vikubwa na vidogo hekta 318 
ambazo zimepimwa na hekta 1,132 zinaandaliwa michoro ya mipango miji.
Alieleza
 katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha imeshatenga hekari 3,266 katika 
maeneo ya Disunyara yenye hekari 466 na kikongo 2,800.
Mhandisi
 Ndikilo anasema wilaya ya Kisarawe kuna hekta 4,500 eneo la Visegese 
ambazo viwanja 291 vyenye ukubwa wa hekari 6 vimepimwa na upimaji 
unaendelea huku eneo la Vihugwe lenye hekari 2,800 linamilikiwa na Kilua
 group co.ltd ambalo kwa sasa lipo kwenye harakati za kupata hati miliki
 .
 
Alisema Bagamoyo ina hekta 12,500 ambapo eneo la EPZA limetengwa hekta 
9,800 ,Mataya hekta 1,200 na Matimbwa hekta 1,500 kwa ajili ya viwanja 
na kusema tathmini na ulipaji wa fidia unaendelea na tayari eneo la EPZA
 wananachi 2,180 walifanyiwa thamini na 1,155 wamelipwa fidia zao.
Wilaya
 ya Mafia alitaja kuna hekta 50 za ardhi katika eneo la Dagoni na huko 
wilaya ya Mkuranga hekari zilizotengwa ni 7,450 kwa ajili ya viwanda 
ambako kijiji cha Dundani kuna hekari 700,Misufini,Mponga ,Kidete na 
Ngalambe 4,000 na Mkiu hekari 1,000.
Rufiji
 imetenga hekta 1,100 za ardhi katika maeneo ya Utunge huko Utete na 
imewekwa kwenye ramani ya mji mdogo wa utete kwa ajili ya viwanda.
Mhandisi
 Ndikilo alisema halmashauri ya Chalinze na Kibiti bado ni changa lakini
 zimeelekezwa kutenga maeneo ya viwanda ili mkoa ufikie adhama 
iliyokusudia .
Hata
 hivyo alieleza kuwa halmashauri nyingine zitaendelea kutenga maeneo ya 
uwekezaji na kuomba wamiliki wa maeneo makubwa wayaendeleze pasipo 
kuyaacha pori na endapo yupo atakaekiuka taratibu za kufutiwa hati zao 
zitafanyika. 
Wakati
 huo huo akizungumzia juu ya miradi kumi iliyopo kimkakati aliitaja kuwa
 ni sanjali na kiwanda cha vigae kiitwacho Goodwill Tanzania ceramic 
co.ltd na Mohammed kilua group ambacho kitakuwa suluhisho katika 
upatikanaji wa nondo.
Mkuu
 huyo wa mkoa alisema kiwanda kingine ni  cha kusindika matunda na 
kuyaongezea thamani cha Sayona fruits kinachotarajiwa kujengwa kijiji 
cha Mboga -Chalinze mwekezaji ni makampuni ya MMI group ambayo 
yatawekeza fedha za kimarekani mil.55.
Kiwanda
 kingine ni cha saruji mamba cement kitakachojengwa kijiji cha 
Magulumatali na Talawanda wilayani Bagamoyo mwekezaji ni MMI group nao 
kibali wameshapata wakati wowote ujenzi utaanza.
Kiwanda
 cha nondo cha MMI kitakajengwa eneo la Zegereni halmashauri ya mji wa 
Kibaha na mradi wa bandari ya nchi kavu na maeneo ya viwanda tayari 
upimaji wa eneo hilo na tathmini ya mazingira na kumtambua mwendeshaji 
wa mradi utakapokamilika umeshafanywa .
Mradi
 mwingine ni wa Eco energy uliopo wilayani Bagamoyo ambao upo kwa ajili 
ya kuzalisha tani 150,000 ya sukari na megawatts 34 za umeme kwa mwaka 
na sasa wanawasiliana  na serikali ili kujua hatua zinaendelea 
kuchukuliwa juu ya mradi huo.
Mhandisi
 Ndikilo ,alisema mbali na mkoa huo kuvutia wawekezaji pia wanasimamia 
na kuhakikisha wananchi wanalipwa fidia sambamba na kuondoa urasimu 
kwenye halmashauri katika mahitaji mbalimbali ya wawekezaji.
Alisema
 wanahakikisha miundombinu ya maji ,umeme na barabara inaboreshwa katika
 maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji 
mkoani Pwani.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni