KONGAMANO LA VIJANA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI MKOANI MWANZA LAFANYA.
Mgeni
Rasmi, Meneja wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mkoani
Mwanza, Damian John Changa, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Biashara,
Viwanda na Uwekezaji, katika ufungaji wa Kongamano la Vijana
Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza lililohitimishwa jana katika
Viwanja vya Gandh Hall Jijini Mwanza.
Alisema
umefika wakati wa vijana kuacha kuilalamikia Serikali huku wakiwa
hawajishughulishi katika kujipatia kipato hivyo kongamano hilo anaamini
limewafungua vijana wengi mkoani Mwanza ambao watatumia elimu ya
ujasiriamali na uwekezaji waliyoipata kutumia fursa zilizopo mkoani
Mwanza ili kujikomboa kiuchumi.
Kongamano
hilo lilifanyika kwa siku mbili kuanzia jumamosi Julai 16,2016 hadi
jana jumapili julai 17,2016 ambapo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania
Youth Enterpreurship Organization pamoja na Taasisi ya Vijana Mwanza
Saccos kwa lengo la kuwawezesha vijana kukutana pamoja kuzungumza,
kujadili na kutathimini kwa pamoja fursa zilizopo mkoani Mwanza na
kuzitumia ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni “Kijana ndio Mhimili wa Upaishaji wa Pato la Taifa, Usisubiri kesho, Fursa ni Sasa”.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Jijini Mwanza, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi
wa Jiji la Mwanza, katika hitimisho la Kongamano la Vijana Wajasiriamali
na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Mwenyekiti
wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza,
akizungumza katika hitimisho la kongamano hilo jana.
Alisema
kongamano hilo limevunga lengo la kuwafikia vijana 1,100 kwani zaidi ya
vijana 2,000 walihudhuria huku pia lengo la kuvifikia vikundi 50 vya
wajasiriamali mkoani Mwanza likivukwa baada ya vikundi 150 kujiandikisha
na kushiriki katika kongamano hilo.
Beatus Kisusi ambae alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kongamano hilo akizungumza wakati wa ufungaji wake jana.
Florah
Magabe ambae alikuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la
Vijana Wawekezaji na Wajasiriamali mkoani Mwanza, alitanabaisha kwamba
lengo ni kongamano hilo kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini ili
kuwafikia vijana wengi zaidi ili waweze kutumia fursa zilizopo katika
kujikwamua kiuchumi.
Mdau
wa Maendeleo Jijini Mwanza ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kahama
Mjini, Jumanne Kishimba, akitoa Mada kuhusu “Watu waliopambana na Maisha
na kufanikiwa katika harakati za kuzalisha mali”.
Mh.Dkt.Antony
Diallo ambae ni Mkurugenzi wa Sahara Media Group, akitoa mada juu ya
“Ujasiriamali na Uwekezaji katika Mkoa wa Mwanza” katika kongamano la
Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Miongoni mwa watoa Mada katika kongamano hilo ambae alitoa mada juu ya “Umuhimu wa Bima katika Biashara”.
Kulwa
William Matolwa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Kanda ya Ziwa,
akitoa mada katika kongamano hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka
hilo Kanda ya Ziwa.
George Binagi-GB Pazzo ambae ni blogger wa BMG, akitoa mada juu ya Matumizi yakinifu ya Mitandao ya Kijamii na Biashara.
Jummy
Peter Masumbuko ambae ni Mratibu Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na
Ufugaji wa Viumbe Maji kutoka Taasisi ya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya
Uvuvi mkoani Mwanza-FETA akitoa mada katika kongamano hilo
Maneno Abubakary kutoka SIDO mkoani Mwanza, akitoa mada katika kongamano hilo.
Donald Kasongi ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Governance Links, akitoa mada katika kongamano hilo.
Mwalimu Beny Mwenda kutoka Chuo cha UKIRIGURU mkoani Mwanza, akitoa mada katika kongamano hilo.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya The Desk and Chair Foundation, Sibtain Meghji, akitoa
salamu za taasisi hiyo ambayo ilifadhiri kwa asilimia kubwa kongamano
hilo ambapo alisisitiza kwamba makongamano ya aina hiyo kufanyika mara
kwa mara ili kusaidia kuwapatia vijana elimu ya ujasiriamali na
uwekezaji huku akisisitiza zaidi pia fursa za makongamano na maonyesho
kama ya Sabasaba pia kufanyika mikoani badala ya kusalia tu Dar es
salaam.
Baadhi
ya waliohudhuria kongamano hilo akiwemo Mwenyekiti wa Machinga Jijini
Mwanza, Masanja Matondo (kushoto), wakifuatilia matukio kwa umakini
zaidi
Baadhi ya wadau wakifuatilia Kongamano hilo akiwemo Katibu wa Machinga Jijini Mwanza (kushoto).
Burudani live kutoka kwa Ramyy Ramulla a.k.a Katoto Ka Mama Rama.
Atrey Kuni ambae ni Afisa Habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliongoza vyema Kongamano hilo.
Wadau katika picha ya pamoja
Mgeni
Rasmi (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa
Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Tazama Hapa Picha za Ufunguzi wa Kongamano Hil
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni