INFANTINO AMSIFU MALINZI
Salamu
 za Infantino zimetolewa na Msimamizi Mkuu wa kozi ya waamuzi nchini, 
Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini akisema, “Infantino ana ripoti zote
 ya namna mpira wa miguu unavyoendeshwa duniani. Anasifu Tanzania kwa  
namna mnavyopiga hatua. Ana ripoti idadi ya makocha walivyokuwa wachache
 na sasa mna makocha wengine wako kwenye kozi.
“Mbali
 ya makocha, leo tuko nanyi waamuzi, ni hatua kubwa ambayo Rais 
Infantino amemsifu Rais wa TFF, Bwana Malinzi,” alisema Henrique.
Henrigue
 aliyeka waamuzi hao kujikita zaidi kusoma namna sheria 17 za mpira wa 
miguu zilivyoboreshwa kwa kuondoa zaidi ya maneno 1,000 ili kuja 
kusimamia vema michezo wa soka huku akiwataka kuwa mahiri wakati wote. 
Henrique anafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na Mark Mzengo kutoka 
Malawi, Felix Tangawarima wa Zimbabwe na Gladys Onyago kutoka Kenya.
Kozi
 za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania sasa ilianza  jana Julai 25, 
2016 kwa waamuzi wenye Beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa
 (FIFA) na waaamuzi waandamizi wanaotarajiwa kuveshwa beji hizo kwa 
majina yao kupendekezwa FIFA kama watapata matokeo mazuri kwenye kozi 
inayoendelea.
Kozi
 ilianza kwa ratiba ya waamuzi wote kuchukuliwa vipimo (physical fitness
 test) kwa kila mwamuzi chini ya wakufunzi hao kutoka FIFA. Baada ya 
vipimo, darasa la waamuzi hao litaanza kwa nadharia na vitendo. Darasa 
hilo litafikia mwisho Julai 29, 2016 kabla ya kuanza darasa la waamuzi 
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya 
StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na makamishna wa michezo 
kwa msimu wa 2016/2017.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni