Mratibu wa Mradi wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Marry Kessy.
Mratibu
wa Mradi wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya la Umoja wa
Mataifa (WHO) , Marry Kessy akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu
usalama barabarani jijini Dar es Salaam, ambapo waandishi wa habari
walipata kujifunza mambo yanayohusu usalama wa barabarani ikiwepo
kupewa ripoti ya ajali ambazo hutokea duniani na Tanzania, umuhimu wa
uvaaji kinga (helment), umuhimu wa uvaaji mkanda kwenye gari, madhara ya
ulevi uendeshapo chombo cha moto na vizuizi kwa watoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi, ASP
Masoko akitoa mada kuhusiana na sheria ya usalama barabarani ya Tanzania
inavyofanya kazi, wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi
wa Usalama wa Barabarani waShirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO)
, Callie Long akitoa elimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo
ya siku moja jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria mafunzo ya usalama barabarani ya siku moja jijini Dar es Salaam ambapo walipata
kujifunza mambo yanayohusu usalama wa barabarani ikiwepo kupewa ripoti
ya ajali ambazo hutokea duniani na Tanzania, umuhimu wa uvaaji kinga
(helment), umuhimu wa uvaaji mkanda kwenye gari uendeshaji vyombo vya
moto na vizuizi kwa watoto
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni