TDL yazindua kampeni ya shinda gari kanda ya ziwa
……………………………………………………………………………………………..
KAMPUNI ya Tanzania
Distilleries Limited (DTL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji cha
konyagi imezindua kampeni ya nunua, uza shinda gari na Konyagi kwa
wasambazaji wa bidhaa hiyo .
Akizungumza katika uzinduzi
wa kampeni hiyo jijini Mwanza juzi, Meneja masoko na Udhamini wa TDL,
George Kavishe, alisema kampeni hiyo itashindanisha magari mawili yenye
thamani ya Sh milioni 98 na itadumu kwa muda wa miezi mitatu ikilenga
kuinua uchumi wa wasambazaji na wauzaji wa bidhaa zao.
Alisema kampeni hiyo itatoa
washindi wawili na kwamba watakaopatikana kwa kuzingatia vigezo husika
watakabidhiwa magari aina ya Eicher 3 Tonne Truck.
“Mshindi atajishindia gari aina
ya Eicher 3 Tonne Truck ambazo zitarahisisha usambazaji wa biashara
yake, hivyo kupitia shindano hili tutakuwa tumeboresha usambazaji wa
biehaa yetu ya Konyagi, wasambazaji na wauzaji wetu kutoka Kanda nne
watashiriki na kila gari ina thamani ya Sh milioni 49.
“Pia kupitia shindano hili kwa
kuwa tunaimani mauzo yataongezeka itatusaidia kuweza kushiriki kutatua
changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa hapa
nchini,”alisema Kavishe.
Meneja wa Chapa ya Konyagi,
Martha Bangu, alisema katika shindano hilo wasambazaji na wauzaji wa
bidhaa hiyo wamewekewa viwango ambapo kiwango cha chini ni katoni 400
na cha juu ni 30, 000 na washiriki wote watakaokidhi vigezo wataingia
kenye droo kubwa ya kupata mshindi inayotarajia kufanyika Oktoba mwaka
huu.
Tunaamini kampeni hii itaongeza
ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongeza kiwango cha ununuzi wa
bidhaa zetu , shindano hili ambalo limeanza Julai mwaka huu litaisha
mwezi Septemba mwaka huu na litajumuisha wasambazaji wetu wote waliopo
mikoa ya kanda ya ziwa, Nyanda za juu kusini , Kaskazini, Pwani na
Kati,”alisema Bangu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni