Diwani
Kata ya Kimara Mhe. Pascal Manota akihamasisha wananchi wa Mtaa wa
Mavurunza Kata ya Kimara kushirikiana na Wataalam wa masuala ya Ardhi
ili kuruhu upimaji wa maeneo yao walipofanya mkutano wa uhamasishaji juu
ya Urasimishaji wa Makazi holela.
Kaimu
Mkurugenzi Urasimishaji Makazi holela Bi. Bertha Mlonda akielezea faida
za urasimishaji katika mkutano wa Uhamasishaji kwa wanachi wa Kata ya
kimara mtaa wa Mavurunza.
Badhi
ya wakazi wa Mtaa wa Mavurunza waliohudhuria mkutano wa Uhamasishaji
kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela, wakiwasikiliza viongozi wa
Serikali za Mitaa (Hawako pichani) pamoja na wataalam kutoka Sekta ya
Ardhi walipokuwa wakitoa elimu kwa wakazi hao.
Hamza
Khatibu, Mkazi wa Mtaa wa Mavurunza akiuliza swali kwa viongozi wa
Serikali za Mitaa na wataalam wa Sekta ya Ardhi walipokuwa katika
mkutano kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela.
Alama
inayotenganisha kiwanja kimoja na kingine inayowekwa na wataalam wa
upimaji kutoka Wizara ya Ardhi, wakishirikia na wataalam kutoka Manispaa
ya Kinondoni.
Wataalam
kutoka Wizara ya Ardhi na Manispaa ya Kinondoni wakiandaa ramani za
maeneo ambayo tayari yamefikiwa kwa ajili ya kupimwa na kurasimisha
makazi holela katika Kata ya Kimara, Mtaa wa Kilungule B.
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imeanza kupima viwanja zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na
Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha
makazi holela.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti Kaimu mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela Bi.
Bertha Mlonda amesema, Uendelezaji Miji ni kwa mujibu wa Sheria ya
MipangoMiji na una faida nyingi kwa wanachi. Alisisitiza kwamba,
Maendeleo ya sehemu yeyote hutokana na miundombinu ya sehemu husika
pamoja na huduma za kijamii zinazopatika.
Mlonda
amewaasa wananchi haswa wa Kata za Kimara na Saranga kutoa ushirikiano
kwa wataalam ambao wameanza kupima maeneo yao ili kuondokana na tatizo
la Makazi Holela kwa wakazi hao kwani upimaji huo utabadilisha taswira
na hadhi ya maeneo yao.
Kwa
sasa Urasimishaji umeanzia katika Kata za Kimara na Saranga, baada ya
hapo yatafuata maeneo yote yenye sifa za urasimishaji katika jiji la Dar
es Salaam, na mikoa yote ya Tanzania. Zoezi hili litakuwa likitekelezwa
kwa awamu kulingana na maeneo yatakavyobainishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni