JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU
 Rais
 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga 
Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na 
Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara 
mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana
 mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya
 basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo 
limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu 
badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na 
kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani 
ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
 
 Rais  Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe 
John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria 
na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa 
hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
  Mkuu
 wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. 
Magufuli kuhusiana na  Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru
 huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA 
ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza 
halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu 
za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
 Wananchi
 wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa  noti ya shilingi 
10,000/- akitaka kumtuza  Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua 
changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri 
wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo 
Jumamosi Julai 30, 2016
Rais
 Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele 
wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga  wakati wa mkutano wake 
wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
PICHA NA IKULU
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni