GOLI LA SAMATTA EUROPA CUP NI GUMZO, KUTOKANA NA UBORA WAKE
Bao alilofunga mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta dhidi ya Buducnost Podgorica katika mechi ya kuwania kucheza Europa Cup, limekuwa gumzo.
Samatta ambaye ni Nahodha
wa timu ya taifa ya Tanzania, alifunga bao hilo na kuihakikishia Genk
ushindi wa mabao 2-0 ikiwa nyumbani katika mechi ya kwanza wakicheza
kwenye Uwanja wao wa Cristal Arena.
Katika
dakika ya 79 Samatta alipewa mpira pembeni mwa uwanja huku ukionekana
kama hauna madhara, akageuka nao kwa haraka na kukimbia kama hatua nje,
huku ikionekana kama atatoa upasi, umbali kama wa mita 25 hivi, akaachia
mkwaju mkali na kufunga bao safi kabisa.
Katika
mitandao mbalimbali ya kijamii, bao hilo limekuwa gumzo huku mashabiki
wa soka wa Genk na wale wa Tanzania wakijadili ubora wake.
Bao
hilo limekuwa muhimu kwa Genk kwa kuwa inajiwekea nafasi nzuri kabla ya
mechi ya marudiano. Lakini nimemtangaza zaidi Samatta kutokana na ubora
wake.
Timu hizo zitarudiana Julai 21, 2016 kwenye Uwanja wa City jijini Podgorica ambapo Genk itakuwa ugenini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni