Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
…………………………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi -MAELEZO -Dar es Salaaam
SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri 
Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la uwekezaji 
litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki 
kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Jijiji Dar es 
Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis 
Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano 
hilo.
Dkt. Issa alisema Serikali 
imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi
 asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu 
katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
“Msukumo mkubwa wa serikali kwa 
sasa ni kuongeza ushiriki katika  uwekezaji unaochochewa na ugunduzi 
mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari  ambao utaweza 
 kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.
Aidha alisema kuwa kutokana 
ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda endelevu, 
Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya 
ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza 
majukumu yake mwezi Novemba mwaka 2015.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji 
Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng’i Issa alisema kuwa katika kongamano
 hilo linatarajia kushirikisha jumla ya wajumbe 350 wakiwemo 
wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Watendaji wa Serikali Kuu na 
halmashauri za Miji na Majiji.
Akizungumzia kuhusu manufaa ya 
kongamano hilo,  Beng’i alisema Watanzania watanufaika zaidi kwa kuwa 
wataongeza ujuzi na uzoefu katika kushirikiana na wafanyabiashara 
wakubwa waliopo nje ya nchi wanaojihusisha na sekta za mafuta, gesi, 
kilimo, fedha, bima, ujenzi na manunuzi ya umma.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni