Serikali yatenga bilioni 1.6 kwa ajili ya uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi.
(Picha zote na Benjamin Sawe- Maelezo)
…………………………………………………………………………………………………..
Benjamin Sawe -Maelezo Dar es Salaam.
Serikali
imetenga Jumla ya shilingi bilioni 1.6 kupitia ofisi ya Taifa ya
Takwimu na wafadhili wametoa shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya
uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi Tanzania
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI Injinia Mussa Iyombe
wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa
sahihi katika serikali za mitaa.
Injinia
Iyombe alisema mfumo huo unalenga kuwa na kanzi data ya watu wote
nchini kiumri, uraia, jinsia, hali ya ulemavu, hali ya elimu, shughuli
za kiuchumi, uhamaji na uhamiaji ikiwa ni pamoja ikiwa na vizazi na
vifo.
“Taarifa
hizi zitaisaidia serikali na wadau wengine kujibu maswali ambayo
wengine tumekuwa tukijiuliza kila siku”.Alsema Injini Iyombe.
Alisema
katika kutekeleza malengo Endelevu ya Maendeleo ya Mwaka 2030 serikal;I
haina budi kuhakikisha wananchi wanaandikishwa katika rejesta ya wakazi
ili iweze kuwafahamu mahitaji yake.
Aliongezea
kuwa mfumo huo utasaidia upatikanaji wa idadi kamili ya wanafunzi
waliopo mashuleni na kiasi gani cha fedha kinachotitajika kupelekwa
shuleni, upatikanaji wa hali halisi ya uandikishaji wa watoto katika
shule za msingi, mahudhurio shuleni na idadi ya walimu na taarifa
nyingine.
Alisema
kwa upande wa TAMISEMI mfumo huo utasaidia kuwagundua wazazi ambao
hawana nia nzuri ya kuwapeleka watoto kuandikishwa kupitia katika kata
zao kwa kutumia Global Positioning System za kaya zao katika ramani.
Akielezea
faida za mfumo huo Injinia Iyombe alisema utaiwezesha serikali kufahamu
idadi kamili ya watu wake kiumri na kijinsia kwa kuwa kazi hiyo itakuwa
endelevu na itafanyiwa kazi kila siku na maafisa watendaji wa vijiji na
mitaa kwa Tanzania nzima kwa kutumia teknolojia ya simu.
Aidha
mfumo huo utaipa fursa Ofisi ya Takwimu ya kuwa na takwimu bora ambazo
zitaipunguzia gharama ya kufanya tafiti za kila baada ya miaka mitatu,
mitano hata kumi ikiwa ni pamoja na kupunguza maswali mengi ambayo
huulizwa wakati wa sensa wa watu na makazi ambayo itafanyika tena hapa
nchini mwaka 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni