MBUNGE WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR ASHIRIKI UJENZI WA TENKI LA MAJI KATIKA JIMBO LAKE
Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
…………………………………………………………………………………………….
Na Maryam Kidiko –Husna Sheha / Maelezo Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal
Kassim Ally amesema changamoto kubwa iliyokuwa inakabili jimbo hilo
zimeaanza kupata ufumbuzi katika kila shehia ndani ya jimbo .
Ameyasema hayo katika ujenzi wa
mnara wa maji ndani ya shehia ya sogea jimbo la magomeni wilaya ya mjini
unguja amesema ujenzi huo ni miongoni mwa ahadi walizozitoa kwa
wananchi wakati wa kampeni .
Amesema changamoto ya maji
ilikuwepo kwa muda mrefu katika shehiya ya sogea jambo ambalo lilikuwa
likirejesha nyuma maendeleo ya shehia hiyo.
“Tumechukuwa juhudi kubwa na
viongozi wenzangu kuanzia madiwani na muwakilishi ili kuona suala hili
linakamilika haraka “ Alisema Jamal.
Aidha amesema wameanzisha mradi wa
visima vya maji sita katika jimbo hilo ili kuweza kupunguza tatizo la
ukosefu wa maji ambalo ni muhimu kwa binaadam kuweza kupata huduma
hiyo.
Hata hivyo ametowa fursa kwa
wananchi wa shehia hiyo kuweka kamati ya visima ili iweze kusimamia
katika mambo mbali mbali yatayovikabili visima hivyo.
Vile vile amefahamisha kuwa visima
hivyo vya wananchi wote hivyo kila mwananchi anahaki ya kutumia na
kuvitunza visima hivyo bila ya kufanya uharibifu .
Pia amewaomba viongozi
watakaochaguliwa kusimamia visima hivyo kuwa na hekma pamoja na busara
ili kuweza kuepusha migogoro kwa wananchi wataopata huduma hiyo.
Sambamba na hayo amewataka
wananchi wa jimbo la magomeni mradi huo utapokamilika waweze kutoa
michango ili kusaidia umeme ambao ndio utaweza kupatikana kwa huduma
hiyo.
Nae Ramadhan Mwadini mzee ambae ni
miongoni mwa wa nanchi wa shehia ya sogea jimbo la magomeni amempongeza
mbunge wa jimbo hilo kwa kuitimiza ahadi aliyoiahidi wakati wa kampeni.
Amewataka viongozi wao wa jimbo kuendelea kutimiza ahadi mbali mbali walizozitoa ili kuweza kuleta maendeleo katika jimbo lao .
Jumla ya visima vinne
vimeshachibwa kati ya visima sita katika jimbo hilo na kila kisima
kimegharimu shilingi milioni saba na laki tano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni