JWTZ NETBALL WANAWAKE WAONYESHA UBABE KWA KIKOSI CHA KVZ WANAUME
pichani) katika Kambi ya Bavuai ikiwa ni maandalizi kuelekea Michuano ya Afrika mashariki kwa majeshi
ya nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika Kigali Rwanda Agosti mwaka Huu. (Picha na Selemani Semunyu)
………………………………………………………………………………..
Na Selemani Semunyu, JWTZ
Mkuu wa mafunzo na Utendaji
Kivita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali
Issa Nassoro amezitaka Timu teule za Jeshi kutobweteka na Ushindi
wanaoupata katika mechi za majaribio wanazocheza.
Kauli hiyo imekuja Mwisho mwa
wiki wakati Timu ya Mpira wa Pete (Netball) Wanawake ya jeshi la
Wananchi wa Tanzania kudhihirisha ubabe wake baada ya kuifunga Timu ya
Mpira wa pete ya Wananume ya kikosi cha Valentia Zanzibar -KVZ kwa
Magoli 36 kwa 24 katika mchezo uliofanyika Mwishoni mwa wiki Visiwani
Zanzibar
Mchezo huo uliofanyika Katika
katika uwanja wa Polisi Bwawani Ulikuwa kivutio kikubwa kutokana na
kuhusisha jinsi mbili tofauti kwa maana ya Wanaume na Wanawawake lakini
pia ukiwa na wachezaji mahiri kutoka katika Timu zote mbili ambao
wamekuwa na majina makubwa katika mchezo huo.
Meja Jenerali Nassoro aliyekuwa
katika Ziara ya kutembelea kambi ya Timu teule za jeshi za mpira wa
Miguu,Pete,Kikapu na Mpira wa Mikono zilizoweka kambi katika Visiwa vya
Unguja Mjini Zanzibar alisema ameridhishwa na kambi licha ya Jitihada
zaidi kuongezwa ili kujihakikishia ushindi.
Alisema anamatumaini Makubwa
historia ya kuweka kambi Zanzibar kutazibeba Timu za Jeshi kwani Timu
mbalimbali zilizowahi kuweka kambi Zanzibar zilipata Mafanikio hivyo
Jeshi na Taifa tunategemea hilo kama eneo zuri kwa kambi ili kujiandaa
vizuri.
“Niliamua kwa Makusudi
kupendekeza kambi kuwa Zanzibar nimekuwa Mchezaji na Mwanamichezo muda
mrefu najua faida za kuweka kambi Zanzibar ukilinganisha na maeneo
mengine kama Dar es Salaam” Alisema Meja Jenerali Nassoro
Katika michezo ya majaribio za
Timu hizo Teule za jeshi Katika Mchezo wa mpira wa Kikapu Timu ya Jeshi
wameifunga Timu ya Mbuyuni kwa Vikapu 104 kwa 58 na kuifanya Timu hiyo
kuendeleza ubabe ikiwa ni mchezo baada ya michezo yake ya Awali
kuzifunga Timu mabingwa wa Mchezo huo kwa Zanzibar.
Timu hizo zilizochezea kichapo
katika Mpira wa Kikapu JWTZ iliifunga Stone Town kwa Vikapu 69 kwa 48
wakati mchezo uliochezwa kabla JWTZ waliifunga polisi kwa Vikapu 68 kwa
49 michezo iliyochezwa katika Viwanja Vya Maisara.
Katika hatua Nyingine Timu ya
Soka ya JWTZ inakumbukumbu ya kuifunga Mafunzo kwa mabao Mawili kwa moja
ikiwa ni mchezo wa marudiano huku mchezo wa Kwanza Timu ya Jeshi ikiwa
imeibuka kwa Ushindi wa mabao Mawili kwa Moja, Katika mchezo Mwingine
JWTZ wameifunga jeshi la Kujenga Uchumi JKU kwa Magoli Mawili kwa Moja.
Katika Mpira wa Mikono JWTZ
wameifunga Vijana Combine kwa Magoli 37 kwa 16 wakati katika Mchezo
mwingine JWTZ waliifunga Zanzibar Warriors kwa Magoli 36 kwa 16.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni