Ntahakikisha Serikali inahamia Dodoma :Rais Magufuli
………………………………………………………………………………………………………
Na. Immaculate Makilika- Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amesema katika kipindi cha uongozi 
wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma.
Amesema hayo leo, wakati 
alipokuwa  akihutibia wajumbe  wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika 
Mkutano Mkuu Maalumu  wa  Chama hicho uliofanyika  mjini Dodoma mara 
baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.
“Nitahakikisha katika awamu ya 
uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi wengine wote nao
 watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma inaweza kukidhi 
mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliendelea kusema 
kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya 
Awamu ya Tano  ameweza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa
 kuanza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Akiongelea maeneo ya utekelezaji 
katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa mpaka sasa Serikali 
imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure kwa shule za Msingi 
na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka zaidi tofauti na 
miaka iliyopita.
Aidha Dkt. Magufuli alisema kuwa 
Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa 
mapato ya serikali hali itakayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma muhimu
 za jamii.
Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza  ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,
Rais Dkt. Magufuli aliongeza kuwa
 Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali ya Uganda wamefanikiwa 
kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima katika ziwa Alberti 
nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta hayo yatasafirishwa 
sehemu mbalimbali duniani na bombahilo  litazalisha zaidi ya ajira 
20,000.
Vile vile, Rais Magufuli alisema 
kuwa Serikali yake imeweza kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa 
umma  na kuweza kuondoa watumishi hewa waliokuwa na waliokuwa wamefikia 
12,500,na  kuongeza kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga fedha za 
matumizi jumla ya shilingi trilioni 29.5, ambapo asilimia 40 ya fedha 
hizo zitapelekwa katika kutekeleza  shughuli za maendeleo.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 
ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000  ulimpitisha Rais Dkt. John Pombe 
Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura 2398  kati 
ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 100.
Rais Magufuli anakuwa  Mwenyekiti
 wa awamu ya Tano baada ya  kupokea uongozi huo kutoka kwa Mwenyekiti wa
 Chama hicho anayemaliza muda wake Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza 
chama hicho kwa kipindi cha miaka 10.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni