HASSANOO AWATAKA WAAMUZI WA MCHEZO WA SOKA WAZINGATIE SHERIA 17 NA KUACHANA NA TAMAA
WAAMUZI wa mchezo wa  soka 
mkoani Pwani wametakiwa kuhakikisha wanachezesha kwa kuzingatia sheria 
17 za mchezo huo na kutoa maamuzi yaliyo sahihi ili wasiwe ni moja ya 
chanzo cha susababisha migogoro n akuvunjika kwa baadhi ya michezo 
wanayokuwa wakichezesha.
Kauli hiyo imetolewa na 
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoani Pwani (COREFA) Hassan Hassanoo 
wakati alipokuwa  akifungua mafunzo kwa waamuzi wa mchezo wa soka wa 
mkoa huo ambayo yaliyofanyika kwenye  uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha 
 Tumbi.
Hassano alisema kwamba mwamuzi 
 wa mchezo wa mpira ni sawa na  na hakimu ambaye anapaswa kutoa maamuzi 
yake kuzingatia sheria kanuni pamoja na taratibu zote ambazo zimewekwa 
katika kuongoza mchezo wa soka ii kuweza kutimiza malengo ya kuweza 
kuuendeleza zaidi kuanzia ngazi za chini hadi za juu.
“Mimi kikubwa ninachowaomba 
waamuzi katika Mkoa wa Pwani tuwe makini sana katika kutimiza majukumu 
yenu, kwani wakati mwingine michezo imekuwa ikivunjika na wengine kutoa 
malalamikoi, kwa hiyo katika hili hakikisheni mnasimamia sheria zote 17 
za mchezo huu wa soka katika Mkoa wetu wa Pwani na sio 
vinginevyo,”alisema Hassanoo.
Aidha aliongeza kuwa suala la 
kuwa mwamuzi wa mchezo wa soko ni wito na  si suala la  biashara kama 
baadhi yao wanavyofanya kama sehemu ya kujiongezea kipato kwani mwamuzi 
anapaswa kuhakikisha mchezo unakwisha salama na hata kama unavunjika 
sababu iwe ambayo ni nje ya uwezo lakini siyo kusababishwa na mwamuzi.
“Kwa hiyo waamuzi mnapaswa 
kujifunza kila mara kwa sababu sheria za soka hubadilika kila mara 
ambapo kwa sasa zimekuwa zikibadilika kama fasheni kwa lengo la kuongeza
 ladha ya mchezo wa soka hivyo lazima muendane na mabadiliko ya sheria 
hizo ili kupunguza lawama ambazo zimekuwa zikitolewa ,” alisema 
Hassanoo.
Aliwataka waamuzi  wasibweteke 
na madaraja waliyopo bali waongeze bidii ili wafike madaraja ya juu na 
kuweza kuchezesha ligi kuu kama walivyo baadhi yao na waweze kufikia 
kuchezesha michezo inayoandaliwa na Mashirikisho ya Soka Afrika CAF na 
Dunia FIFA na mkoa utaendelea kutoa mafunzo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya 
waamuzi ambaye alisoma risala ya waamuzi hao Kasule ambogo alisema kuwa 
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolipwa posho
 zao kwa wakati ambapo zamani walikuwa wakilipwa hata kabla ya mchezo.
Ambogo alisema kuwa pia 
changamoto nyingine ni kukosa mafunzo hayo ya kujikumbusha sheria za 
soka kwa muda mrefu hivyo kusababisha waamuzi kushindwa kupanda 
 madaraja kwa wakati na kuksa hata sifa za kuweza kuchezesha katika ligi
 kuu ya Tanzania bara.
KOZI hiyo ambayo ilifanyika kwa
 siku mbili kwa kuwashirikisha waamuzi  wapatao 60 kutoka maeneo mbali 
mbali ya Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Pwani.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni