KOKA:AWAASA WALIMU WAKUU NA WATENDAJI KUTUNZA MADAWATI YA MISAADA
……………………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MBUNGE
wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ,amewataka walimu wakuu wa
shule za msingi na watendaji wa mitaa na kata katika halmashauri ya Mji
huo, kusimamia na kuhakikisha wanayatunza madawati mapya yanayotolewa na
wadau mbalimbali ili kuondoa tatizo la ubaha wa madawati mashuleni.
Amesema mwalimu mkuu ama mtendaji ambae atazembea kusimamia suala hilo basi atawajibishwa .
Koka
aliyasema hayo ,wakati akikabidhi madawati 537 yenye thamani ya zaidi
ya mil. 37 yaliyotolewa na serikali ikiwa ni mgao wa wabunge nchini
kwenye sehemu ya posho zao .
Alieleza
kuwa serikali haitakuwa tayari kuona madawati yanayotolewa na
wahisani,wadau na yale yaliyotengenezwa na wadau hayafuatiliwi wala
kupewa matunzo.
“Ni
wajibu wa kila mtendaji,walimu na wanafunzi wenyewe kuwa wasimamizi
kutokana na fedha zilizotumika ni kodi za wananchi hivyo lazima zilindwe
kwa faida ya watoto hao “alisema Koka.
Aidha
Koka alisema awali wanafunzi walikuwa wanapata shida na kero wakati wa
kusoma ambapo wengine walikuwa wakikaa chini na kuchafuka kwa vumbi na
kuandikia chini hivyo kushindwa kupata elimu yao kwenye mazingira yasiyo
bora.
Alisema
serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Magufuli ,iliona iweke
mkakati madhubuti wa kuchangia madawati na viti na meza katika shule za
msingi na sekondari ili kuondoa kero ya upungufu uliokuwepo miaka ya
nyuma.
Koka
alisema kuwa ni jambo la lazima na sio hiari kwa walimu wakuu kuwa moja
ya wakaguzi na wasimamizi wakuu wa madawati hayo ili hata kama yatakuwa
yameharibika kidogo yatengenezwe na si kuyaacha hadi yaharibike .
Nae
mwakilisha wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha Jennifer
Omolo,afisa elimu wa halmashauri ya Mji huo,Maajabu Mkanyemka alisema
kabla ya agizo la rais kulikuwa na mahitaji ya madawati 9,162.
Alieleza hadi kufikia June 30 walikuwa tayari wametengeneza na kukarabati madawati 6,979 hivyo kwasasa wana upungufu wa 2,183.
Maajabu
alisema hadi sasa madawati yaliyopatikana ni 2,500 kati ya mapungufu
ya 2,183 huku 572 yakiwa yanatengenezwa na mara yatakapokamilika
kutakuwa na ziada ya madawati 312 hivyo kutarajia tatizo la madawati
kubaki historia mjini hapo.
Alisema katika upande wa shule za
sekondari mahitaji ya meza yalikuwa 7,032 vilivyopo ni 6,041 na kubakia
na upungufu wa meza 991 huku viti walivyokarabati na kutengeza ni viti
6,099 kukiwa na upungufu wa viti 933 hadi sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni