WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO HATARINI KUFA KWA KUKOSA DAMU
Kamanda wa jeshi la zima
moto na uokoaji mkoani Pwani, mrakibu msaidizi,Goodluck Zerote
,akichangia damu ,katika zoezi lililoendeshwa na jeshi hilo ,kuchangia
damu hospital ya rufaa ya Tumbi.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WATOTO chini ya umri wa miaka mitano mkoani Pwani wako kwenye hatari ya kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu.
Hayo yalielezwa na afisa
muuguzi wa wa kitengo cha damu salama hosptali ya rufaa ya Tumbi
,Elisia Towo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi
la utoaji damu kwa hiari lililokuwa likiendeshwa na jeshi la zima moto
na uokoaji mkoani hapo.
Alisema watoto wenye
umri huo wamekuwa wakiongoza kwa kukosa damu kutokana kuugua ugonjwa wa
malaria lakini pia kucheleweshwa kuwahishwa hospitali mapema.
“Tumekuwa
tukiwahamasisha wazazi katika mihadhara mbalimbali kuhakikisha
wanawawahisha watoto hosptali pindi wanapoona dalili ya homa ama
malaria badala ya kuwaleta wakiwa wameshachoka na ugonjwa”, alisema
Towo.
Alieleza kuwa kundi
jingine lililo hatarini ni wakina mama wajawazito ambao nao wamekuwa
wakipata tatizo la ukosefu wa damu ama wakihitaji kufanyiwa upasuaji .
Towo amesema watu wengine ni majeruhi wa ajali ambao hawatabiriki kwani ajali hutokea bila ya kuwa na taarifa.
Muuguzi huyo alisema
kutokana na mahitaji hayo hosptali ya rufaa ya Tumbi inahitaji damu
nyingi zaidi ambapo kwa sasa iliyopo ni unit 25 ambayo ni ndogo
ikilinganishwa na matukio ya mara kwa mara ya ajali.
“Kwa siku tunakusanya
unit 12 hadi 20 na mahitaji yetu kwa mwezi ni kuanzia unit 250 hadi 300,
bado damu haitoshi, nawaomba wananchi wa mkoa wa Pwani wajitokeze
kuchangia damu kwa hiari ili waweze kuokoa maisha ya watanzania wenzetu
wanaohitaji damu”, alisema Towo.
Afisa uhusiano wa jeshi
la zima moto na uokoaji SGT Harrison Mkonyi alisema zoezi hilo ni
endelevu na kuwa lengo ni kuhakikisha jeshi hilo linatimiza kauli mbiu
yake ya kuokoa maisha na mali kwa vitendo.
Kamanda wa jeshi la
zimamoto na uokoaji mkoani Pwani Mrakibu msaidizi Gudluck Zerote
,alisema hii ni mara ya kwanza kwa jeshi hilo mkoani humo kuchangia
damu.
Kamanda Zerote alisema
kutokana na kuwa kwa mara ya kwanza wamechangia damu hosptali ya Tumbi
unit 12, na kuwa watachangia baada ya miezi mitatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni