Kilele Maadhimisho Siku ya vijana Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku
ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika
Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari.
Mhe Mavunde amebainisha kuwa
Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa
uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo
Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi
wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika
shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi
ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili
kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.
Akizungumzia maadhimisho hayo
Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki
shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya
Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania tutasherekea siku ya
Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa
tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na
Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa na siku ya Vijana
Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991
Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha
fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku
ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu
ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni