MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM
Meja
Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani
(kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya
Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam
leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa
kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa
Septemba Mosi mwaka huu.
Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
Msaada ukitolewa.
Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.
Watoto wakipata msaada huo.
Watoto wakipokea msaada.
Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.
Na Dotto Mwaibale
JESHI
la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na
sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa utoaji wa msaada huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es
Salam , Meja Dora Kawawa alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya
kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ).
“Tumeamua
kushiriki shughuli za kijamii kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa
ni kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake
kitakuwa Septemba mosi mwaka huu” alisema Kawawa.
Ofisa
Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice
Lawrance alishuru JKT kwa msaada huo na kueleza ni muhimu sana kwa
watoto hao na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa
bora la kesho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni