KATIBU MKUU WA MALIASILI NA UTALII, MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI AMEWATAKA MAJANGILI WATAFUTE KAZI NYINGINE
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
 na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akifunga mafunzo maalum ya 
kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la 
Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori
 kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika 
kupambana na kukabiliana na  majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Balozi wa Marekani nchini 
Tanzania, Mark Childress akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu 
ya ya kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba
 la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari 
wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu 
katika kupambana na kukabiliana na  majangili. ( Picha na Lusungu 
Helela- MNRT)
Askari wanyamapori wakionesha kwa 
vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la
 Akiba la Rungwa  Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna 
ya kupambana na majangili  wakati  wakiwakamata majangili ( Picha na 
Lusungu Helela- MNRT)
Askari wanyamapori wakionesha kwa 
vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la
 Akiba la Rungwa  Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna 
ya kupambana na majangili  wakati  wakiwakamata majangili ( Picha na 
Lusungu Helela- MNRT)
Baadhi ya askari wanyamapori 
waliohitimu mafunzo wakiwa kwenye paredi jana katika Pori la Akiba la 
Rungwa mkoani Singida,  Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori 
kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika 
kupambana na kukabiliana na  majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya 
Usimamizi wa wanyamapori Tanzania ( TAWA) Childress akizungumza wakati 
wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana  na ujangili kwa Askari 
wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo 
hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia 
kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na  majangili.
 ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Askari wanyamapori wakionesha kwa 
vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la
 Akiba la Rungwa  Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna 
ya kupambana na majangili  wakati  wakimkama ta jangili akiwa 
amejisalimisha yeye mwenyewe. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
…………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
 na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi   ametoa  wito kwa  watu 
wanaojihusisha na vitendo vya ujangili waache kazi hiyo  baadala yake 
watafute kazi nyingine zitakazoweza kuwaingizia vipato halali kwa 
 kufanya hivyo wataweza kujiepusha kutiwa nguvuni na askari wanyamapori 
waliobobea kwa kazi hiyo.
Milanzi alitoa wito huo  jana 
   wakati wa  akifunga  mafunzo maalumu ya kupambana na Ujangili kwa 
askari wanyamapori  katika pori la akiba la Rungwa mkoani Singida 
yaliyofadhiliwa na Marekani na yaliyotolewa na Kikosi maalum cha 
wanajeshi kutoka Marekani.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni 
muhimu sana kwa askari wanyamapori  ili kuendelea na kukabiliana na 
wimbi kubwa la ujangili kwa kuwa majangili wasasa wanatumia silaha za 
kisasa tofauti na majangili wa  zamani ambao walikuwa wakitumia upinde 
na mishale.
Aliongeza kuwa majangili  wa sasa 
ambao askari wanyamapori wamekuwa wakikabiliana nao maporini  ni wale 
ambao  wanatumia silaha za kivita  hiyo ni lazima askari wetu  wapewe 
mafunzo ya hali ya juu ili waweze kukabiliana nao.
Aidha Katibu Mkuu, Milanzi alisema
 Wizara imejipanga kuhakikisha suala la ujangili linakwisha ambapo kituo
  kingine cha mafunzo ya kijeshi kwa askari wanyamapori cha Mlele 
kilichopo Mkoani Katavi kimeanzishwa mbali na  vyuo vya  Pasiansi na 
Mweka, Likuyu Sekamaganga ambavyo pekee ndivyo vilivyokuwa vikitoa 
mafunzo kwa askari wanyamapori.
Aliongeza kuwa,  kwa sasa Serikali
 imejipanga kwa kushirikiana na Interpol  kuhakikisha kuwa hatakamatwa 
jangili tu aliyehusika  kuua mnyama porini bali mtandao wote utakamatwa 
na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria mahali popote.
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo
 hayo, Milanzi alisema mafunzo hayo yamejikita kuwasaidia kupambana na 
majangili, magaidi pamoja na majambazi ambapo wao ndo watu wa kwanza 
kukumbana nao wakiwa porini kwani ndiko wanakotumia kujificha  kwahiyo 
ujuzi walioupata umewaongezea ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo 
kwenye maeneo yao.
Aliwataka pia wahitimu hao kufanya
 kazi kwa kujituma wasiishie tu kusherekea kumaliza mafunzo bali 
waonyeshe kwa vitendo hii itasaidia na kuipa ari Marekani pamoja na 
 Asasi za kimataifa zenye lengo la kusaidia nchi katika vita dhidi ya 
Ujangili.
Kwa upande wake  Balozi wa 
Marekani nchini Tanzania, Mark Childress amewataka wahitimu wazingatie 
mafunzo waliyopata kwa kuyafanyia kazi ili Pori la Akiba la Rungwa liwe 
sehemu salama kwa wanyamapori wanaopatikana katika pori hilo.
Ameahidi kuwa nchi yake itaendelea
 kuisaidia  Tanzania kwa kuwa suala la ujangili bado ni kubwa 
linalohitaji ushirikiano wa pande zote ili liweze kutokomezwa.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni