Watanzania washauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili kuutangaza Utamaduni
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi 
Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo 
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye 
Dira Tanzania (UWARIDI) katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es
 Salaam Agosti 25,2016.
Rais wa Umoja wa Waandishi wa 
Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw. Hussein Tuwa akitoa neno wakati
 wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar 
es Salaam Agosti 25,2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi 
wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Ibrahim Gama akitoa maelezo kwa 
mgeni rasmi kuhusu Umoja wao wakati wa uzinduzi wa Umoja wa huo katika 
ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi 
Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo 
akionesha cheti cha usajili wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira 
Tanzania (UWARIDI) mara baada ya kuuzindua umoja huo huo katika ukumbi 
wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa 
Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) wakimsikiliza 
mwakilishi wa mgeni rasmi Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani 
Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo(hayupo 
pichani) katika uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space
 Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi 
Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na 
Michezo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamojja na viongozi na 
wajumbe wa kamati kuu ya Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira 
Tanzania (UWARIDI) mara baada ya uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa 
Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Baadhi ya vitabu vya Riwaya vilivyoandikwa na wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).
……………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Watanzania wameshauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili katika ulimwengu wa uandishi ili kuutangaza Utamaduni wa nchi.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es 
Salaam na Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka 
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa uzinduzi wa Umoja 
wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).
Mkurugenzi amesema kuwa kwa 
kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na kuenzi juhudi za 
kuenzi na kuendeleza juhudi za watetezi za masuala ya lugha wa masuala 
ya Lugha na Utamaduni wa mtanzania.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia 
Baraza la Kiswahili la Taifa imeandaa kanuni za Sheria ya BAKITA ya 
mwaka 1967 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni ambayo 
itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili waandishi hapa nchini pamoja 
na haki zao  katika kuendeleza fani mbalimbali za Lugha.
“Katika azma ya kukuza na 
kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa  Rais wetu  Mhe.Dkt John 
Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika hotuba zake 
mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat  Shani.
Kwa upande wake mmoja ya wajumbe 
wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa  katika risala yao kwa mgeni rasmi 
amesema kuwa umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania(uwaridi)  
wameamua kutafuta njia ya kurudisha, kutetea, kulinda na kuipandisha 
heshima yetu kama waandishi na heshima ya kazi zetu zote.
“Tumeamua kutafuta mbinu za kuweza
 kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu zinatambuliwa rasmi kiserikali na
 kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja wetu ambao utakuwa na sauti 
katika kutetea haki za waandishi na kazi zao alisisitiza Bi. Matilda.
umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye
 Dira Tanzania (uwaridi) umeanzishwa kwa lengo la kuwatetea waandishi wa
 Riwaya nchini ili waweze kunufaika na kazi zao.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni