Msanii Nigeria atoa msaada katika Kituo cha Kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, Kigamboni Community Center
Mwanzilishi wa Kampuni ya
Mahusiano ya Umma, LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji,
Jagabana maarufu YCEE (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka
kulia ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt na
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center
Mbwana Msangule.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tinny
Entertainment kutoka Nigeria Arokodare Timilehin akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji,
Jagabana maarufu YCEE (wa tatu kutoka kushoto) leo Jijini Dar es
Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha
Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny
Entertainment Oladaro Pratt.
Msanii Omo Alhaji, Jagabana
maarufu YCEE kutoka Nigeria akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ziara yake katika Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Uhusiano
wa Umma ya LAS Consultancy ya Jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto
ni Mwanzilishi wa Kampuni ya LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana,
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center
Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia mkutano baina ya uongozi wa LAS Consultancy walipokuwa
wakimtambulisha msanii kutoka Nigeria Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE
ambaye yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kutembelea Vyombo vya Habari.
Msanii Omo Alhaji, Jagabana
maarufu YCEE kutoka Nigeria akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi milioni moja kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha
Kigamboni Community Center Mbwana Msangule(kushoto) leo Jijini Dar es
Salaam Katikati ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro
Pratt.Msanii hyo yupo nchini kufuatia ziara yake kwa Vyombo vya Habari
inayoratibiwa na Kampuni ya Mahusiano ya Umma ya LAS Consultancy.
Picha na Frank Shija, MAELEZO.
……………………………………………………………………..
Na Sheila Simba,Maelezo
Msanii wa muziki kutoka nchini
Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada wa shilling
million 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu
cha Kigamboni Community Center(KCC).
Akizungumza katika ukumbi wa Idara
ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa ujio wa msanii
huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa msaaada huo katika
kituo hicho kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji
maalum ya kila siku wawapo kituoni hapo.
“Ametoa msaada huo kutokana na
faaida anayopata katika kazi zake usanii ili kukuza vipaji na kujenga
upatikanaji wa elimu wa elimu kwa jamii hasa ya watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi,”alisema Salha
Akizungumza baada ya kupokea
msaada huo Mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule,amesema kuwa kituo
chake kinalea watoto hao ili kuwasaidia kuondokana na maisha magumu
yanayowakabili.
“msaada huu utasaidia sana
kwasababu kituo kina watoto 14 wanaoishi kituoni hapo na wengine
wanakuja na kurudi makwao,na nashukuru sana kwa msaada huu kwani ni
sanii wa kwanza kutoka msaada,nawaomba pia wasanii wa ndani kijitokeza
kutoa msaada”alisema Mbwana
Kwa upande msanii huyo amesema
kuwa amekuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuonana na wasanii
wengine wakubwa wa Tanzania huku akiwataja Diamond na Ali Kiba,ameongeza
kuwa amefurahi pia kuktana na mashabiki wake ambao amekua wakichati
kupitia mitanzandao ya kijamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni