UVCCM WILAYA YA ARUSHA YAMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI
Na Mahmoud Ahmad Arusha
BARAZA la umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi ,UVCCM,
wilaya ya Arusha, limempongeza rais John Magufuli kwa hatua
anazozichukua za utendaji na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya
serikali .
Hayo yameelezwa leo na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya
Arusha, Martini Mnisi, alipokuwa akihutubia kwenye kikao cha baraza kuu
la Umoja wa vijana wilaya ya Arusha, lililofanyika ukumbi wa ccm, mkoa
na kusisitiza vijana kumuunga mkono rais Magufuli.
Mnisi, amesema hivi karibuni kumetokea upotoshaji kuwa rais
anawachukia matajiri na huo ni uongo ambao haufai kuvumiliwa na Baraza
linaukemea ,ukweli ni kwamba rais hawachukii matajiri bali wanaokwepa
kulipa kodi hao ndio maadui wa serikali.
Amesema baraza litatoa ushirikiano kwa Rais ambae ni
mwenyekiti wa CCM, taifa kwa hatua za kuwatumbua watu wasio waadilifu
na wazembe ili kurejesha heshima ,hadhi na nidhamu ambayo ilikuwa
umetoweka miongoni mwa watumishi wa umma na chama cha mapinduzi.
Mnisi ,akawataka mbunge wa jimbo la Arusha na meya wa jiji
la Arusha na kuacha kumtuhumu mkuu wa wilaya kwa madai anawaingilia
katika utendaji wao jambo ambalo sio kweli bali wanapaswa wasome katiba
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili waelewe majukumu na wajibu wa
mkuu wa wilaya.
Amesema meya na madiwani wa jiji la Arusha, wameshindwa
kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ushuru wa magari katika baadhi ya
maeneo na sasa wanaandaa hujuma ya kuipaka matope serikali ionekane
utaratibu wa kurejesha vyanzo vya mapato kutoka kwa wazabuni kuwa hauna
manufaa.
Awali akifungua kikao hicho Kamanda wa vijana wa UVCCM,
wilaya ya Arusha, Karim Mushi , amewataka vijana ambao ni jeshi la CCM,
kujipanga upya ili kutokurejea makosa yaliyosababisha jimbo na kata zake
kupotea .
Amesema vijana wanapaswa kutanguliza masilahi ya chama na
sio masilahi binafsi kwa kuwa msingi wa chama cha mapinduzi ni kufanya
kazi zake kwa kujitolea hivyo watangulize chama mbele masilahi binafsi
baadae.
Mushi, akawataka vijana hao kuhakikisha wanasimamia kwa
karibu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM, na kuhakikisha fedha za
rais Magufuli, zinazotolewa kwenye ngazi za mitaa na vijiji zinawafikia
walengwa kwa kuwa fedha hizo ni za serikali hivyo zisigeuzwe kuwa ni
mtaji wa kisiasa kwa madiwani wa Arusha.
Amesema inauma sana kuona Cham cha mapinduzi katika jimbo
la Arusha kugeuzwa kuwa upinzani ambapo sasa ni sawa na utumwa, na hiyo
inatokana na wana ccm kutokukitendea haki chama cha mapinduzi kwenye
uchaguzi mkuu .
Munishi, amesema umefika wakati wana ccm kujitafakari upya kwa kuhakikisha hawarejei kwenye makosa yaliyotokea
Kwenye kikao hicho baraza linafanya uchaguzi wa wajumbe
watatu wa baraza hilo kujaza nafasi zilizoko wazi sanjari na kujaza
nafasi ya mjumbe mmoja kutoka Vijana kwenda wazazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni