KAMANDA SIRRO ATANGAZA KIAMA KWA WANANCHI WATAKAO ANDAMANA SEPTEMBA MOSI JIJINI DAR ES SALAAM
 Kamanda 
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon
 Sirro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake 
Dar es Salaam leo, wakati akitangaza kiama kwa mwananchi yeyote 
atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania 
yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 
 Kamanda Sirro akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Magari 
ya polisi yenye zaidi ya askari 80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha Kati,
 yakielekea Vikindu kwa ajili ya Operesheni saka majambazi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askari wa
 kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha 
Polisi cha Kati kuelekea Vikindu kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu
 wanaotuhumiwa kwa ujambazi.
……………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
KAMANDA 
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon
 Sirro ametangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano 
Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha 
Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
“Jeshi la
 polisi mkoa wa Dar es Salaam tumejipanga vizuri siku hiyo nawaomba 
wananchi wasidhubuti kujitokeza kuandamana siku hiyo kwani watakiona cha
 moto” alisema CP Sirro.
Sirro 
alisema tayari jeshi hilo lina taarifa za kiinteligensia kuwa kuna 
vijana wanapewa fedha kwa ajili ya kuandamana na kufanya fujo Septemba 
mosi.  
Aliwasihi wananchi hasa vijana kutoingia barabarani Septemba mosi na kuwaachia wachache wenye nia ya kuletafujo.
“Ni rai 
yangu wale wananchi wazalendo wan chi hii wasiopenda kupambana na jeshi 
lao la polisi ambalo linawalinda na kulinda mali zao siku hiyo wasiingie
 barabarani,” alisema.
Aliwakaribisha
 wanao taka kuingia barabarani na kupambana na jeshi hilo na kuwa 
watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
“Sisi 
tupo vizuri na tupo imara hasa kwa wale wanaopenda kuvunja sheria kwa 
makusudi wata wajibika kwa mujibu wa sheria, hivyo suala la utiiwa 
sheria bila shuruti ni la msingi sana,” alisema Sirro.
Alisema 
jeshi hilo limejiandaa kwa wananchi wachache ambapo alibainisha 
 wananchi wengine hawana haja na maandamano hayo huku akibainisha vijana
 wachache wenye shida kupewa fedha na viongozi kwa lengo la kuandamana.
“Jiulize 
hiyo  40,000 unayo pewa kuingia barabarani na matokeo yake ukavunji kama
 mguu hiyo  40,000 ina thamani gani kwani… kwa hiyo mimi kama kiongozi 
wenu wa jeshi la polisi na sisitiza na ninaelekeza tuwaache wale wenye 
 sababu zao binafsi waingie barabarani,” alisema.
Katika 
hatua nyingine Kamanda Sirro alisema askari zaidi ya 80 wa kikosi 
maalumu cha kupambana na uhalifu wameondoka kwenda vikindu na maeneo 
mengine wilayani Mkuranga mkoani Pwani kufanya operesheni ya kuwasaka 
watu wanaodhaniwa kujihusisha na ujambazi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni