Wananchi Zanzibar watakiwa kulipia huduma ya maji
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa 
kulipia huduma ya maji kwa wakati ili kuweza kupata huduma hiyo kwa 
ufanisi zaidi na kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na Afisa 
Uhusiano wa  Mamlaka ya Maji Zanzibar  (ZAWA) Zahour Suleiman  Ofisini 
kwake  Msikiti Mabuluu Mjini Zanzibar wakati akitoa maelezo kuhusiana na
 ulipaji wa huduma ya maji.
Amesema maji ni moja ya huduma 
muhimu katika maisha ya wananchi  hivyo ni muhimu  kuhakikisha 
yanapatikana muda wote  na suala la  kulipia huduma hiyo ili iwe 
endelevu  ni jambo la msingi.
Afisa huyo amefahamisha kuwa 
badhi ya wananchi wamekuwa na  mwamko mdogo katika kulipia huduma ya 
maji na  kusababisha  Mamlaka kukosa uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa 
ufanisi.
Aidha amesema kuwa kwa sasa 
huduma hiyo inaelekea kuzidiwa kutokana na kukuwa kwa harakati za 
kimaendeleo hasa kwa matumizi ya kilimo ambacho kinatumia maji mengi 
 ukilinganisha na matumizi ya majumbani.
Afisa huyo amefahamisha kuwa 
wameanzisha  utaratibu  wa kupita katika maeneo kwa lengo la kutoa elimu
 kuhusiana na  umuhimu wa kulipia maji na  wale watakaoshindwa kuufahamu
 mpango huo Mamlaka huwapa onyo na baadae kusitishwa kupata huduma.
Sambamba na hayo Zahour 
amewashauri wanajamii kufuata sheria bila ya kushurutishwa kwa kulipia 
maji kwa wakati ili kuipa uwezo Mmlaka ya maji kutekeleza wajibu wake wa
 kuwapatia  wananchi huduma hiyo kama kawaida.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni