KAMPUNI YA UDALALI YA YONO YAINGIA MKATABA WA KIMATAIFA NA KAMPUNI YA BIDDERS CHOICE YA AFRIKA KUSINI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scholastika
Christian Kevela (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es
Salaam leo (hawapo pichani), mkataba wa kimataifa walioingia na Kampuni
ya Bidders Choice ya Afrika Kusini wa ushirikiano kwa ajili ya kufanya
mnada wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa
dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji
wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scholastika
Christian Kevela (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kulia
ni Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela. Nyuma kushoto ni Ofisa wa
kampuni hiyo, Salome Sabas na kulia ni Abdrew Kevela.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Udalali ya Yono Auction Mart imeingia mkataba wa ushirikiano na
Kampuni ya Bidders Choice ya Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya mnada
wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa
dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga .
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni hiyo, Scholastika Kevela alisema wameingia mkataba huo Agosti
24 mwaka huu ambapo watafanya minada ya kuuza mitambo ya zamani ya
kampuni ya Acacia kwa njia ya mtandaoni.
Alisema
kampuni ya Bidders Choice imewapa tenda ya kufanya minada ya mitambo
ya zamani ya madini mbalimbali ambayo inatakiwa kutolewa na kuwekwa
mipya.
“Hivyo
tunategemea kwenda kwenye mgodi wa dhahabu Bulynhulu kuangalia ni
mitambo gani inatakiwa kupigwa mnada ili iwekwe mingine,”alisema Kevela.
Mwenyekiti
wa Kampuni hiyo,Stanley Kevela alisema kampuni yake ilipata tuzo ya
ufanyaji kazi kwa ubora ambayo imesaidia nchi ya Afrika Kusini kutoa
mkataba huo wa kimataifa ambao haujawahi kufanyika nchini kwa kampuni
nyingine ya udalali isipokuwa ya Yono.
Alisema
kutokana na utendaji wao kuwa mzuri hivyo wanatarajia kuanzisha chuo
cha madalali kitakachosaidia serikali kukusanya mapato ya kutosha.
“Hiki
chuo cha madalali kikianzishwa kitaleta maendeleo kwenye jamii yetu na
jamii wataelewa umuhimu wa kukusanya kodi hivyo taifa litapata mapato
mengi, alisema Kevela.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni