Vituo viwili vya Redio vyafungwa kwa muda.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa 
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akitoa tamko la kufungia vituo
 viwili vya redio ambavyo ni Kituo cha Redio Five Arusha  na Magic  FM 
Dar es Salaam kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es
 Salaam, kutokana na  kukiuka Kanuni za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 
2005 kwa kurusha hewani vipindi vyenye maudhui ya uchozezi,na Kushoto ni
 Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo vya Habari Bw. Jamal  Zuberi wa 
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Baadhi ya waandishi wa Habari 
wakifuatilia tamko alilokuwa akitoa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na
 Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) la kufungiwa kwa Redio
  Five  Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam leo Agosti 29,2016 Jijini
 Dar es Salaam.
………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Serikali yafungia vituo viwili vya
 redio nchini kutokana na kurusha hewani taarifa za kichochezi 
zinazoweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Tamko la kufungwa kwa vituo hivyo 
vya  redio limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, 
Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa 
akizungumza  na waandishi wa habari.
Aidha,Waziri Nape alivitaja vituo 
hivyo kuwa ni Kituo cha Redio Five cha Arusha na Kituo cha Redio Magic  
FM Dar es Salaam na alisisitiza kuwa utekelezaji wa tamko hilo unaanza 
leo tarehe Agosti 29, 2016 mara baada ya kutangazwa.
“Uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo 
umefikia baada ya kujiridhisha kuwa kipindi cha MATUKIO kilichorushwa 
tarehe 25 Agosti ,2016 muda wa 02:00 usiku hadi 03:00 usiku  na Kituo 
cha Utangazaji cha  Redio Five  Arusha na kipindi cha cha Morning  Magic
 katika kipengele cha KUPAKA RANGI kilichorushwa tarehe 17 Agosti, 2016 
kati ya saa 01:00 asubuhi na saa 02:00 asubuhi vilikuwa na maudhui ya 
uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa amani na hivyo kukiuka masharti ya
 kanuni ya 5 (a),(b),(c) na (d) pamoja na Kanuni ya Huduma za Utangazaji
 (Maudhui) za mwaka 2005”, alisema  Waziri Nnauye.
Waziri huyo mwenye dhamana na 
vyombo vya habari nchini alisema vituo hivyo vimefungiwa kwa muda 
usiojulikana na ameelekeza  Kamati ya Maudhui kuviita vyombo hivyo na 
 kuwasikiliza kwa kina zaidi na kumshauri hatua zaidi za kuchukua kwa 
mujibu wa Kanuni za Utangazaji za mwaka 2005.
Pamoja na hayo Waziri Nape 
alivitahadharisha  vyombo mbalimbali  vya habari ,kutoshawishika kuvunja
 Sheria na Kanuni  zinazoongoza tasnia ya Habari ili kulinda heshima ya 
tasnia ya habari  na kuhakikisha nchi inabaki na Amani.
Hata hivyo  Sheria ya Mamlaka ya 
Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003  Kifungu cha 28 (1) kimempa Mamlaka 
Waziri wa mwenye dhamana na masuala ya Habari kufungia vyombo vya habari
 vinavyoweza kurusha hewani habari za uchochezi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni