Lukuvi afanya ziara eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya Fundi gereji katika Mtaa 
wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Bw. 
Mohamed Ali akielezea sababu za wao kuvamia eneo la Kilichokuwa kiwanda 
cha nguo cha KiliTex kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 
Mhe. William Lukuvi (hayupo pichani).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza kwa makini Afisa 
Ardhi toka Manispaa ya Ilala Bw. Furaha Mwakapalila akielezea historia 
ya eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex ambalo kwa sasa 
limevamiwa na mafundi magari wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es 
Salaam.
Afisa Tarafa wa Ukonga Bw. 
Jeremiah Makorere akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya waziri huyo 
kubaini migogoro mbalimbali ya ardhi katika eneo la Pugu Jijini Dar es 
Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa 
wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao 
wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa 
wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao 
wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa 
wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia 
eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick 
Factory (KIBRICO) wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya 
ardhi katika eneo la Pugu.
Mwenyekiti ya Kamati ya malalamiko
 ya wakazi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam
 ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha
 Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) Bw. Deus King΄ung΄alo akisoma risala 
kwa niaba ya wakazi hao wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya Waziri huyo 
kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni